| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Al Hilal ya Sudan yaweka historia kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Rwanda
Huu ni msimu wa kwanza kwa Al Hilal kushiriki ligi hiyo ambapo msimu uliopita ilishiriki Ligi ya Mauritania na kuchukua ubingwa.
Al Hilal ya Sudan yaweka historia kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Rwanda
Kwa sasa, huu unakuwa ubingwa wao wa 3 kwenye nchi tatu tofauti tofauti./Picha:Wengine

Klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan imeweka historia kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda, baada ya kuifunga Gasogi United kwa mabao 2-1, zikiwa zimesalia mechi tatu kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2025/2026.

Huu ni msimu wa kwanza kwa Al Hilal kushiriki ligi hiyo ambapo msimu uliopita ilishiriki Ligi ya Mauritania na kuchukua ubingwa.

Kwa sasa, huu unakuwa  ubingwa wao wa tatu kwenye nchi tatu tofauti tofauti.

Licha ya kushinda ubingwa huo, klabu hiyo bado haijapata tiketi ya moja kwa moja ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, kwani italazimika kurudi nchini Sudan kushindana katika mashindano ya ligi ndogo ambayo yataamua ni timu zipi zitakazostahili kuiwakilisha Sudan katika mashindano ya CAF kati ya vilabu msimu ujao.

Al Hilal na Al Merrikh zinashiriki ligi ya Rwanda kutokana na sababu za kiusalama nchini mwao.

CHANZO:TRT Afrika Swahili