Uturuki imetangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia la FIFA 2026, huku kocha Vincenzo Montella akichagua mseto wa wachezaji wa kimataifa wenye uzoefu na vipaji viinavyoibuka kwa ajili ya mashindano hayo yatakayochezwa Marekani, Canada, na Mexico.
Mechi hizo zitaanza Juni 11 hadi Julai 19, Uturuki ikirudi tena kwenye michuano ya Kombe la Dunia baada ya kufuzu kupitia mashindano ya Ulaya.
Nahodha Hakan Calhanoglu anaongoza kikosi hicho, pamoja na mchezaji mahiri wa Real Madrid Arda Guler, mshambuliaji wa Juventus Kenan Yildiz na mlinzi Merih Demiral.
Montella amewaita magolikipa watatu: Altay Bayindir, Mert Gunok na Ugurcan Cakir.
Safu ya ulinzi, Abdulkerim Bardakci, Eren Elmali, Caglar Soyuncu, Mert Muldur, Ferdi Kadioglu, Merih Demiral, Ozan Kabak, Samet Akaydin na Zeki Celik wamechaguliwa.
Nafasi ya kiungo inajumuisha Hakan Calhanoglu, Ismail Yuksek, Kaan Ayhan, Orkun Kokcu na Salih Ozcan.
Safu ya mashambulizi Uturuki ina Arda Guler, Baris Alper Yilmaz, Yunus Akgun, Can Uzun, Deniz Gul, Irfan Can Kahveci, Kenan Yildiz, Kerem Akturkoglu na Oguz Aydin.
Baadhi ya wachezaji makinda, ikiwemo Can Uzun na Deniz Gul, pia wamejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho huku Uturuki ikijiandaa kuonesha tena umahiri wake chini ya kocha Montella.
Ratiba ya mechi
Uturuki itaanza mechi zake za Kombe la Dunia dhidi ya Australia Juni 14 katika uwanja wa BC Place mjini Vancouver.
Nyota hao wa Hilali kisha watapambana na Paraguay Juni 20 huko San Francisco Bay kabla ya kukabiliana na wenyeji Marekani Juni 26 huko Los Angeles.
Ratiba ya mechi za Uturuki (GMT):
• Juni 14: Australia vs. Uturuki – 0400 (Vancouver)
• June 20: Uturuki vs. Paraguay – 0300 (San Francisco Bay Area)
• June 26: Uturuki vs. Marekani – 0200 (Los Angeles)
Uturuki inalenga kupita zaidi ya hatua ya makundi na kufanikiwa zaidi ya historia waliyoiweka 2002 ambapo walimaliza nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia la FIFA.



























