| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Cameroon kurudisha nafasi ya makamu wa rais ili kumrithi rais iwapo kutatokea dharura
Kikao cha mabunge mawili lile la taifa na Seneti siku ya Alhamisi kilianza kutathmini muswada wa mabadiliko ya katiba ambao utarudisha tena nafasi ya makamu wa rais kukamilisha muhula wa rais iwapo kutakuwa na dharura ya kufanya hivyo.
Cameroon kurudisha nafasi ya makamu wa rais ili kumrithi rais iwapo kutatokea dharura
Rais Paul Biya, 93, amekuwa rais wa Cameroon tangu 1982. / Reuters
tokea saa limoja

Kikao cha mabunge mawili lile la taifa na Seneti siku ya Alhamisi kilianza kutathmini muswada wa mabadiliko ya katiba ambao utarudisha tena nafasi ya makamu wa rais kukamilisha muhula wa rais iwapo kutakuwa na dharura ya kufanya hivyo.

Rais Paul Biya, 93, amekuwa kiongozi wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati yenye utajiri wa mafuta na kakao tangu 1982, na kwa sasa kiongozi mwenye umri mkubwa zaidi duniani.

Mabadiliko makubwa ya katiba nchini Cameroon yalifanyika mwisho mwaka 2008 ambapo yaliondoa ukombo wa mihula ya rais.

Serikali inasema nafasi ya makamu wa rais itahakikisha mpango 'endelevu'

Serikali inasema nafasi ya makamu wa rais inalenga kuhakikisha kuendelea kwa uongozi wa taifa pale endapo rais hatokuwepo.

Kulingana na muswada huo, mamlaka ya kumteua na kumfuta kazi makamu wa rais atakuwa nayo rais, na atahudumu kipindi ambacho hakitozidi muhula wa rais wa miaka saba.

Muswada huo unaeleza kuwa makamu wa rais atakamilisha sehemu ya muhula wa rais iliobakia iwapo kiongozi wa nchi atafariki dunia, kujiuzulu, au kutokuwa na uwezo kabisa.

Pia unasema kaimu rais hatoweza kuanzisha marekebisho ya katiba au kugombea urais.

Nafasi ya makamu wa rais iliondolewa 1972

Chama tawala cha Cameroon (CPDM) kina wajumbe wengi katika mabunge yote mawili, kufanya kuidhinishwa kwa muswada huo kuwa rahisi.

Nafasi ya makamu wa rais ilikuwepo hadi 1972, ilipoondolewa kufuatia kura ya maoni kuhusu katiba.

CHANZO:TRT Afrika Swahili