| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Morocco iko imara kuliko Paraguay: Kocha wa Ufaransa Deschamps
Kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps, ametoa wito wa wachezaji wake kuwa makini katika mashambulizi wakati wanapoikabili Morocco siku ya Alhamisi katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia.
Morocco iko imara kuliko Paraguay: Kocha wa Ufaransa Deschamps
Didier Deschamps ametaka Ufaransa kuwa makini zaidi dhidi ya Ufaransa mechi ya robo fainali. / Reuters

Ufaransa imefunga magoli mengi kwenye michuano hiyo, magoli 14 lakini kocha Didier Deschamps ametoa wito kwa wachezaji wake siku ya Jumatano kuwa makini zaidi katika ushambuliaji wanapokabiliana na Morocco katika mechi ya robo ya fainali siku ya Alhamisi.

Mechi hiyo ni ya marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022, wakati Ufaransa ilipomaliza ndoto ya kihistoria ya Morocco nchini Qatar, lakini wakati huu timu hiyo ya Afrika Kaskazini siyo wageni lakini ni kikosi ambacho kimeimarika na kina nia ya kupata ushindi.

"Lazima tuwe thabiti, kwa kweli kabisa," Deschamps aliwaambia waandishi wa habari. "Katika maeneo yote timu zote zina uwezo mkubwa."

"Tuko vizuri lakini tunahitaji kuimarika zaidi. Wakati mwingine unapata nafasi sita alafu unafunga magoli mawili tu na wakati mwingine unapata nafasi sita na unafunga mabao mawili. Ni muhimu kuwa thabiti zaidi."

CHANZO:TRT Afrika Swahili