| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
FIFA yamuunga mkono Rais Gianni Infantino baada ya mkutano wa dharura Morocco
Shirikisho hilo limekiri kuhusu 'makosa' kuhusu mpango tata wa mapendekezo ya uwekezaji $20 bilioni wa Kombe la Dunia ambao sasa wameachana nao, wakiongeza kuwa ‘hawatokubali maadili yao yatatizwe tena’
FIFA yamuunga mkono Rais Gianni Infantino baada ya mkutano wa dharura Morocco
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Gianni Infantino.

Viongozi waandamizi wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wameeleza kumuunga mkono Rais Gianni Infantino siku ya Jumatano baada ya mkutano mjini Rabat, Morocco. Viongozi hao walikuwa wanajaribu kutuliza mambo kutokana na mpango wa uwekezaji wa nje wa Dola bilioni 20 ambao kwa sasa FIFA imeachana nao.

Katika taarifa, Katibu Mkuu wa FIFA Mattias Grafstrom na wajumbe wa Kamati Kuu wa Shirikisho hilo "walisisitiza kumuunga mkono kikamilifu Rais wa FIFA Gianni Infantino," huku Infantino akieleza kumuunga kwake katibu mkuu na usimamizi wa FIFA.

"Uongozi wa juu wa FIFA una imani kuwa matokeo ya mkutano huu utaimarisha utawala wa FIFA, kusaidia kurudisha imani na kutuwezesha kuandaa mashindano makubwa pamoja na kukabiliana na changamoto zijazo kwa pamoja na uwazi wakati tukiendelea na majukumu yetu ya kuimarisha soka duniani," taarifa hiyo ilisema.

Mkutano huo uliangazia mapendekezo tata, ambapo FIFA ilikuwa inaangalia uwezekano wa kuuza haki za matangazo na usimamizi wa Kombe la Dunia kabla ya kuacha na mpango huo ulioshutumiwa na wengi.

FIFA ilisema kuwa "watu walikiri makosa," ikiongeza kuwa "haikuwa nia ya Baraza la FIFA na Mashirikisho ya FIFA kuhisi kutengwa kutoka katika mchakato huo na kwamba mchakato huo ulitakiwa kushughulikiwa kitofauti."

Bodi ya usimamizi imesema kuwa barua tofauti ya kuomba radhi kwa makosa yaliyofanyika imetumwa kwa wajumbe wa Baraza la FIFA na mashirikisho ya mataifa na kwamba tathmini itafanyika na matokeo kuwasilishwa kwa baraza wiki ijayo.

CHANZO:َAA