| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Timu nne za Afrika zafuzu kwa Kombe la Dunia kwa Wanawake
Algeria, Morocco, Cameroon na Malawi wamefuzu kwa Kombe la Dunia kwa Wanawake 2027 nchini Brazil.
Timu nne za Afrika zafuzu kwa Kombe la Dunia kwa Wanawake
Malawi imefuzu kwa Kombe la Dunia kwa Wanawake kwa mara ya kwanza. X @COSAFAMEDIA

Algeria, Morocco, Cameroon na Malawi wamefuzu kwa Kombe la Dunia kwa Wanawake 2027 nchini Brazil.

Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcon) nchini Morocco pia yanatumika kama daraja la kufuzu kwa Kombe la Dunia mwakani. Timu zote zilizofika hatua ya nusu fainali tayari zimepata tiketi hiyo.

Mataifa manne yaliyofungwa kwenye mechi za robo fainali za Wafcon - Ghana, Cote d'Ivoire, Nigeria na Afrika Kusini - bado yana nafasi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia kupitia mchakato wa mechi za mtoano.

Siku ya Alhamisi,Cote d'Ivoire inakabiliana na Ghana na Nigeria kukipiga na Afrika Kusini ambapo washindi wawili katika mechi hizo wataelekea kwenye mashindano ya mtoano ya mataifa 10 kati ya mabara mwezi Novemba na Disemba.

Kati ya timu hizo 10 katika hatua ya mtoano, tatu zitafuzu kwa Kombe la Dunia, ambalo linaanza tarehe 24 Juni na kumalizika 25 Julai mwakani.

CHANZO:TRT Afrika Swahili