Uturuki ilipata matokeo mazuri dhidi ya Marekani, kwa kuwafunga 3-2 katika mechi yao ya mwisho ya Kundi D ya Kombe la Dunia katika uwanja wa Los Angeles nchini Marekani.
Marekani ilianza mechi kwa kasi, huku Auston Trusty akiingiza goli katika dakika ya tatu katika mechi hiyo ya Alhamisi.
Uturuki ilisawazisha muda mfupi baadaye. Mchezaji nyota wa Real Madrid Arda Guler akifunga goli lake la kwanza la Kombe la Dunia.
Shuti la karibu
Kipindi cha pili, Marekani ikasawazisha katika dakika ya 49 kupitia Sebastian Berhalter, ikiwa goli lake la kwanza kimataifa.
Wakati mechi inakaribia kumalizika, Uturuki ilipata goli la ushindi kupitia Kaan Ayhan dakika ya 90+8 na shuti kali la karibu, ukiwa ni ushindi wao wa kwanza kwenye michuano hii.
Kocha wa Uturuki Vincenzo Montella anasema timu yake inarejea nyumbani wakiona fahari baada ya ushindi wao katika mechi ya mwisho.
Montella aliwapongeza wachezaji kwa kuonesha vipaji vyao, uwezo licha ya kufahamu kuwa tayari wameondolewa kwenye mashindano hayo na mbele ya mashabiki wengi wa Marekani.
"Tunaweza kwenda nyumbani tukiona fahari," Montella alisema.
Kwa matokeo ya mechi hiyo, Marekani imemaliza kileleni mwa Kundi D, na kufuzu kwa hatua ya mtoano, huku Utuuki ikimaliza wa mwisho, na kuyaaga mashindano hayo.
Marekani itacheza dhidi ya Bosnia na Herzegovina katika raundi ya timu 32.















