Mwamuzi wa soka wa Somalia Omar Abdulkadir Artan ambae alizuiwa kuingia nchini Marekani kusimamia mechi za Kombe la Dunia, amepata mapokezi ya kishujaa nchini mwake Somalia, huku uamuzi wa Marekani wa kutomruhusu refa huyo ukiendelea kuibua hisia tofauti.
Artan amesema, ndoto yake ilikuwa ni kuwa miongoni mwa marefa watakaochezesha Kombe la Dunia, ingawa ndoto yake imekatizwa.
