Kombe la Dunia la FIFA 2026 sio tu kuhusu mataifa yanayotafuta taji lenye hadhi kubwa zaidi katika kabumbu, pia kuna suala la familia.
Kwa mara ya kwanza, kuna ndugu kadhaa wanaoshiriki michuano hii, huku baadhi yao wakiwakilisha nchi tofauti.
Miongoni mwa hali ya kuvutia lakini si ya ajabu ni kuwa mchezaji Nico Williams anacheza timu ya taifa ya Hispania huku kaka yake Iñaki Williams akiwa na Ghana. Wamechagua timu za taifa tofauti licha ya kukulia pamoja Hispania na hata kucheza kwenye klabu moja ya Atletico Bilbao.
Kisha kuna mshambuliaji wa PSG Désiré Doué ambaye yeye anawakilisha Ufaransa katika Kombe hili la Dunia, kaka yake Guéla Doué anavaa uzi wa Cote d’Ivoire, na wanaweza kuwa kundi la pili la ndugu kukabiliana kwenye Kombe la Dunia wakiwa wanawakilisha mataifa tofauti.
Beki wa Arsenal Jurrien Timber yuko na timu ya Uholanzi pamoja na pacha wake Quinten Timber.
Mabeki wa Ufaransa Lucas na Theo Hernández wanaipambania nchi yao Ufaransa huku Curaçao ikiwa na fursa ya kuwatanguliza ndugu Leandro na Juninho Bacuna katika michuano hii mikubwa.
Simulizi zao zinaangazia jinsi uhamiaji, uraia pacha na uhusiano wa familia unavyoonesha mtazamo wa kandanda ya kisasa.
Iwe wanacheza bega kwa bega au wakivaa jezi za nchi tofauti, ndugu hawa wanaongeza msisimko wa kipekee wa familia kwenye Kombe la Dunia ambalo tayari linaweka historia.











