| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Rais wa Senegal Faye asema Waziri Mkuu Sonko kuendelea kuwepo iwapo atatekeleza majukumu 'vizuri'
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye anasema chama tawala kiko kwenye ati ati ya kusambaratika lakini kiongozi wake, Waziri Mkuu Ousmane Sonko, atabaki kwenye wadhifa iwapo "atafanya kazi yake vizuri."
Rais wa Senegal Faye asema Waziri Mkuu Sonko kuendelea kuwepo iwapo atatekeleza majukumu 'vizuri'
Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye na Waziri Mkuu Ousmane Sonko. / TRT Afrika Français

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye anasema chama tawala kiko kwenye ati ati ya kusambaratika lakini kiongozi wake, Waziri Mkuu Ousmane Sonko, atabaki kwenye wadhifa iwapo "atafanya kazi yake vizuri."

Matamshi ya Faye, yaliyooneshwa kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumamosi, yanakuja huku kukiwa na uvumi kuwa muungano wa wawili hao kisiasa unayumba,huku taifa hilo la Afrika Magharibi lilikabiliwa na changamoto za kiuchumi kutokana na deni na athari za vita vya Iran.

Sonko alikuwa mwanasiasa maarufu wa upinzani wakati wa serikali iliopita. Alizuiliwa kugombea urais 2024 kutokana na kupatikana na hatia na akamchagua Faye, mwandani wake wa muda mrefu na mwanachama wa chama cha Pastef, kuchukua nafasi yake.

Kisha Faye akamteua Sonko kuwa waziri mkuu. Tangu wakati huo, dalili za kutoelewana zimejitokeza kati ya wawili hao.

'Maslahi ya Senegal kwanza'

Mwezi Machi, Sonko alisema yuko tayari kukiondoa chama chake ndani ya serikali na kurejea kwenye upinzani kama Faye atakiuka dira ya Pastef.

“Kama wanachama wa Pastef hawatobadilisha mkondo, chama kiko kwenye hatari ya kusambaratika," Faye alisema siku ya Jumamosi, akiongeza kuwa chama kiliungwa mkono kote kwa sababu watu wa Senegal walifahamu kuhusu ilani yake kuliko maslahi ya watu binafsi.

Pia alieleza kuwa na haki ya kumteua na kumtimua waziri mkuu.

"Madamu (Sonko) waziri mkuu yupo madarakani, ina maana anafanya kazi vizuri, na mimi naridhika na hilo. Hata hivyo, siku ambayo sitoridhika na utenda kazi wake, nitayapa kipaumbele maslahi ya Senegal kwanza," alisema.

CHANZO:TRT Afrika Swahili