| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan: Uhuru wa kidijitali ni sehemu muhimu ya usalama wa taifa
Uhuru kamili hauwezi kutenganishwa na uhuru wa kiteknolojia, amesema Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.
Erdogan: Uhuru wa kidijitali ni sehemu muhimu ya usalama  wa taifa
Rais Recep Tayyip Erdogan anasema uhuru wa kidijitali hauwezi kutenganishwa na usalama wa taifa . / / Anadolu Agency
tokea masaa 4

Uturuki inaona uhuru wa kidijitali katika sekta ya ulinzi kuwa sehemu isiyotenganishwa ya usalama wake wa taifa, alisema hayo Rais wa Uturki siku ya Jumanne, akiongeza akiongeza kuwa: “Uturuki sasa inabuni teknolojia yake yenyewe, inatengeneza programu zake yenyewe, na inasafirisha bidhaa zake kote duniani.”

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Sancar — chombo kipya cha majini kisicho na rubani — Erdogan alisema: “Sancar inaongeza uwezo wetu wa mifumo isiyo na rubani baharini, ikiimarisha usalama wetu, ufanisi, na uwezo wa ufuatiliaji.”

Sancar, ambacho ni chombo cha kwanza cha majini kisicho na rubani cha aina yake, kimetengenezwa na kampuni ya ulinzi ya Uturuki, Havelsan, kwa kushirikiana na kiwanda cha meli cha Yonca Shipyard, kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya majeshi ya kisasa ya majini.

Havelsan imetumia mfumo wa misheni wa ADVENT ROTA (Network Supported Data Integrated Combat Management System).

Wakati wa hafla hiyo, miundombinu mipya ya Havelsan pia ilizinduliwa rasmi.

Erdogan alisisitiza kuwa uwekezaji wa Havelsan ni mwendelezo wa hatua za kimkakati zitakazoongeza uwezo wa jumla na athari za mfumo mzima wa sekta ya ulinzi ya Uturuki.

Aliongeza kuwa ukamilishaji wa jengo la Havelsan utalifanya kuwa kituo kikubwa zaidi barani Ulaya cha uzalishaji na ujumuishaji wa teknolojia za usimulizi wa kimfumo (simulation).

Erdogan alisema kuwa nchi haiwezi kuzungumzia mustakabali salama ikiwa programu zake si za kitaifa, kwa kuwa uhuru kamili hauwezi kutenganishwa na uhuru wa kiteknolojia.

Aidha, alieleza kuwa Uturuki sasa inatumia mfumo wa kugundua, kutambua, na kushambulia kwa kutumia teknolojia yake ya ndani na ya kitaifa.

CHANZO:Anadolu Agency