| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Wafungwa wasiopungua 11 wafariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika jela DRC
Mlipuko wa kipindupindu katika gereza moja magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umesababisha vifo vya wafungwa wasiopungua 11 na kuwaambukiza wengine kadhaa, wizara ya sheria imesema Jumatatu.
Wafungwa wasiopungua 11 wafariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu katika jela DRC
Wafungwa wasiopungua 11 wamefariki kutokana na kipindupindu nchini DRC, mamlaka zilithibitisha Machi 30, 2026. / Reuters
30 Machi 2026

Mlipuko wa kipindupindu katika gereza moja magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umewaua wafungwa wasiopungua 11 na kuwaambukiza wengine kadhaa, wizara ya sheria ilisema siku ya Jumatatu.

Mlipuko huo wa kipindupindu ulithibitishwa Machi 27 katika gereza kwenye mji wa Mbanza-Ngungu mkoa wa kati wa Kongo, karibu kilomita 150 kutoka mji mkuu Kinshasa, Waziri wa Sheria Guillaume Ngefa alisema katika taarifa.

"Kwa bahati mbaya kufikia leo, wafungwa wasiopungua 11 wamefariki dunia kutoka na maradhi hayo, huku wengine 74 wakiwa wameambukizwa ikiwa ni miongoni mwa idadi ya wafungwa 800," alisema.

Maafisa wa afya wamepelekwa gerezani huko kuwatibu wagongwa na kuchukuwa hatua za kinga, ikiwemo chanjo, aliongeza.

Alitangaza kuwa hatua za usafi zitazingatiwa, ufuatiliaji wa ubora wa maji ya kunywa na kwa muda hawatoruhusu wafungwa wapya kupelekwa katika gereza hilo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili