| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Wadukuzi wadukua maombi ya kazi 450,000 nchini Afrika Kusini
Takwimu nchini Afrika Kusini zinaeleza kuwa udukuaji ulilenga mifumo ya maombi ya kazi ya watu.
Wadukuzi wadukua maombi ya kazi 450,000 nchini Afrika Kusini
Mashambulizi haya yanaongeza matukio ya udukuzi ya ransomware dhidi ya taasisi za serikali Afrika Kusini. / Getty Images
30 Machi 2026

Taasisi ya Takwimu ya Afrika Kusini (Stats SA) imekabiliwa na udukuzi, huku wadukuzi wakidai kuiba maombi ya kazi zaidi ya 450,000 katika mifumo hiyo, ikiwa moja ya matukio makubwa ya uhalifu wa mitandaoni kwa taasisi ya serikali ya Afrika Kusini.

Udukuzi huo umeathiri idara ya rasilimali watu na hasa maombi ya watu ya kazi, kuzua wasiwasi kuhusu usalama wa taarifa binafsi za watu zilowasilishwa kupitia mtandao huo wa kutafuta ajira serikalini.

Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Risenga Maluleke alithibitisha kuwa rekodi hizo zinahusiana na idara ya rasilimali watu. “Kilichodukuliwa ni taarifa zaidi za idara ya Raslimali watu; tuna mfumo wa kutuma maombi ya kazi kwa njia ya mtandao, ambapo watu wanaweza kufikia kutoka eneo lolote lile,” alisema.

Kundi la XP95 ransomware limedai kuhusika na linataka kulipwa, likiweka muda wa mwisho wa kufanya hivyo kuwa Aprili 20, shirika la habari la serikali SABC limeripoti.

‘Udukuzi kwa majukwaa ya maombi ya kazi’

Maluleke anaeleza kuwa udukuzi unaweza kuwa ulikabili mifumo ya taasisi ya tawkimu ya Afrika Kusini kupitia majukwaa ya maombi ya kazi. “Huenda wakawa wametumia vibanda vya kutoa huduma za intaneti; na pengine walitumia simu zao, ambazo haziko salama – na kwa mantiki hiyo, ni taarifa zao tu tulizonazo. Kwa hiyo, ni taarifa za watu ambazo ziko hatarini.”

Taasisi ya takwimu Afrika Kusini (Stats SA) inasema kuwa inafanya kazi na mamlaka na kuarifu shirika la kuratibu taarifa huku uchunguzi ukiendelea.

CHANZO:TRT Afrika and agencies