| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mchina akamatwa akiwa anapiga picha ndege za kijeshi za Marekani
Tianrui Liang, anadaiwa kukutwa akipiga picha ndege hizo katika kambi ya Nebraska.
Mchina akamatwa akiwa anapiga picha ndege za kijeshi za Marekani
Kambi hiyo inafahamika kwa kuhifadhi vifaa vya kiuchunguzi na ndege zingine za kivita kama vile RC-135 na E-4B Nightwatch./Picha:Wengine

Raia mmoja wa China amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy baada ya kubainika kuwa alikutwa akipiga picha ndege za kijeshi za Marekani karibu na kambi ya kijeshi iliyoko Nebraska.

Tianrui Liang amekutwa na hatia ya kukiuka sheria za nchi hizo ambazo zinapiga marufuku upigaji picha kwenye ngome za ulinzi.

Mamlaka za Marekani zinasema kuwa, Liang alikamatwa Aprili 7 wakati akijaribu kupanda ndege, siku chache baada ya kutolewa kwa hati yake ya kukamatwa.

Kulingana na hati iliyotolewa na FBI, mashushushu hao, walipata taarifa kuhusu mtu mmoja aliyeonekana na kamera katika viunga vya kambi hiyo ya jeshi la anga.

Kambi hiyo inafahamika kwa kuhifadhi vifaa vya kiuchunguzi na ndege zingine za kivita kama vile RC-135 na E-4B Nightwatch.

 

CHANZO:AA