tokea saa limoja
Jeshi la Somalia na walinzi wa amani wa Umoja wa Afrika wamemkamata kamanda mkuu wa Al-Shabaab katika operesheni ya pamoja katika eneo la Shabelle.
Salaad Cusmaan Macalin, maarufu kama Sahm, alikamatwa kaskazini magharibi mwa eneo la Mubarak.
Kamanda huyo alijiunga na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab mwaka 2009.
Baada ya kufanyiwa mahojiano, Salaad alikiri kuwa mshirika wake kutoka Kenya, anayejulikana kama Ismaaciil, alikuwa anapanga njama za kufanya shambulio la kujitoa mhanga.
Katika operesheni hiyo, mmoja wa washukiwa aliyetambulika kama Salman, alifanikiwa kutoroka.
Kwa zaidi ya miaka 16 sasa, kikundi cha Al-Shabaab kimejihusisha na mapambano dhidi ya serikali ya Somalia, mara kwa mara kikishambulia raia na vikosi vya ulinzi.
CHANZO:AA















