Tume ya Umoja wa Afrika inasema haina nia ya kulaumu Misri au nchi yoyote jirani kwa yanayojiri ndani ya Ethiopia baada ya Misri mapema kukanusha kuhusu taarifa ya AU kuhusu uhasama kwenye kanda hiyo.
Tume hiyo inasema imetafakari kuhusu taarifa ya kukanusha ya Misri ya Oktoba 1, ambayo inataka Ethiopia, Eritrea na Misri kuepusha uhasama, na kujadiliana ili kuondoa tofauti zao kupitia diplomasia.
“Hakuna popote” ambapo taarifa hiyo ililaumu nchi jirani kuhusu yanayoendelea Ethiopia, tume hiyo ilisema.
Ilisema kuwa wito huyo ulitolewa baada ya maafisa wa ubalozi kutimuliwa kutoka jijini Addis Ababa, Cairo na Asmara na lengo lilikuwa kuzuia kutoelewana, au kuzidisha uhasama ambao ungesababisha ukosefu wa usalama katika kanda.
Kuunga mkono uhuru wa mipaka ya nchi
Tume hiyo ilisisitiza kuwa dhamira yake ya kuheshimiwa kwa uhuru wa mipaka na umoja wa mataifa wanachama wa AU pamoja na msingi wa kutoingilia masuala ya ndani ya nchi.
Ilisisitiza kuwa taarifa zake zililenga kuimarisha amani, usalama na uthabiti kote katika bara la Afrika na haikuwa na nia ya kuzungumzia yanayojiri ndani ya nchi za mataifa wanachama.
Misri ilipinga taarifa ya tume hiyo siku ya Jumapili, huku vyanzo rasmi vikiieleza kuwa “juhudi hasi” za kuhusisha Misri katika masuala ya ndani ya Ethiopia.
Tume ya Umoja wa Afrika inasema kuwa inathamini uhusiano wake na Misri, ukilieleza taifa hilo kama mmoja ya waasisi wa umoja huo na mshirika muhimu katika kuimarisha amani, usalama na maendeleo kote Afrika.



















