| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Uturuki yaongeza sitisho la safari za ndege kuelekea Mashariki ya Kati
Nchi hiyo imesitisha safari za kwenda Iran, Iraq, Syria, Lebanon, Jordan mpaka Machi 9.
Uturuki yaongeza sitisho la safari za ndege kuelekea Mashariki ya Kati
Ndege za Turkish Airlines./Picha:Reuters
tokea masaa 8

Uturuki imeongeza sitisho la kutosafiri katika baadhi ya mataifa ya Mashariki ya Kati hadi mpaka Machi 9 kutokana na kuongezeka kwa hatari ya mgogoro unaoendelea katika eneo hilo, kulingana na Waziri wa Uchukuzi wa Uturuki.

Kupitia ukurasa wa NSosyal, Abdulkadir Uraloglu alisema kuwa mamlaka za nchi hiyo bado zinaendelea kufuatia hali hiyo, akianisha kufungwa kwa anga za Iran, Israel, Iraq, Qatar, Bahrain, Kuwait, na Syria, isipokuwa kwa Aleppo.

Aliongeza kuwa, safari chache zinaendelea katika maeneo ya Oman, Jordan na Saudi Arabia, huku hali katika Falme za Nchi za Kiarabu ikifuatiliwa kwa umakini.

Kulingana na waziri huyo, hapo awali, Shirika la Ndege la Uturuki lilisitisha safari zake wa kwenda Iran, Iraq, Syria, Lebanon na Jordan hadi Machi 6 kutokana na hofu za kiusalama.

Hata hivyo, aliongeza kuwa sitisho hilo limesogezwa mbele hadi Machi 9 kwa mashirika ya ndege yaliyo chini ya Turkish Airlines, yakiwemo AJet, Pegasus na SunExpress.

Aliongeza kuwa Pegasus ilikuwa imeondoa safari zake za kuelekea Iran mpaka Machi 12, huku Turkish Airlines ikisitisha safari kama hizo hadi Machi 20.

Uraloglu alisisitiza kuwa kutokana na tathimini ya kiusalama, safari za ndege za kwenda Qatar, Kuwait, Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu, hazitokuwepo siku ya Ijumaa.

"Kwa kuongezea, kutakuwa na ndege 4 za shirika la Iraq zitakazokuwa zimepaki katika Uwanja wa Ndege wa Istanbul, 2 katika uwanja wa Mugla, moja kwenye uwanja wa Dalaman na nyingine katika uwanja wa ndege wa Ankara Esenboga," alisema Uraloglu.

Aliongeza kuwa, ndege mbili za Turkish Airlines na Pegasus zipo katika uwanja wa ndege wa Tehran, huku kukiwa na moja Iraq.

Wakati huo huo, kufuatia tukio la ndege nyuki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nakhchivan, ndege mbili za Shirika la Ndege la Azerbaijan, zililazimika kubadili safari na kutia katika uwanja wa Igdir Sehit Bulent Aydin, ambapo abiria walitumia usafiri wa barabara.