Uturuki imesema kuwa Iran inakabaliwa na mashambulizi haramu, ikilaani mashambulizi hayo yanayofanywa kwa pamoja kati ya Marekani na Israel.
Akizungumza jijini Ankara siku ya Jumatatu, Msemaji wa chama cha AK Omer Celik, aliweka wazi kuwa mashambulizi hayo hayakuwa ya haki, na yalikwenda kinyume na sheria za kimataifa, akionya kwamba mashambulizi hayo yatakuwa na athari kubwa katika majadiliano ya kidiplomasia.
“Diplomasia isitumike kama kivuli cha kupanga mashambulizi,” alisema. “Iwapo mashambulizi bado yanaendelea, basi hiyo itakuwa gheresha tu.”
Celik alitumia fursa kutuma salamu zake za rambirambi kwa watu wa Iran, kufuatia vifo vya watu wasia na hatia, ikiwemo shambulizi dhidi ya shule ya msingi na viongozi wa kidini, siasa na kijeshi.
Kuhatarisha usalama wa kanda
Celik alionya kuwa, jitihada za kuwashambulia viongozi wa nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa na kujadili mabadiliko ya uongozi wa yataharisha usalama wa kanda.
Kulingana na Celik, jitihada za kutaka kubadilisha uongozi zimewahi kusababisha vita vya wenyewe na ukosefu wa amani.
Kuchukua hatua
Huku akionesha mshikamano na watu wa Iran, Celik aliitahadharisha Iran kuhusu kuongeza wigo wa vita hivyo.
Kulingana Celik, Uturuki inafuatilia kwa ukaribu hali hiyo, pamoja na hatari ya kuongezeka kwake.
Mamlaka za Uturuki zimesema kuwa zinachukua tahadhari katika mambo kadhaa; ikiwemo uingiaji wa watu kutoka mpaka na Iran, uchumi na usalama wa Waturuki nje ya nchi.
“Taasisi zetu zinafanya kila aina ya uratibu,” alisema Celik, akisisitiza kuwa balozi za nchi hiyo zinaendelea kutoa msaada kwa Waturuki walioko kwenye mataifa yaliyoathirika.













