| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Hotuba ya Rais Erdogan UN yachapishwa kama kitabu kwa lugha tatu
Vitabu hivyo kinafikisha ujumbe wa Rais wa Uturuki kuhusu mauaji ya halaiki ya Gaza, migogoro duniani na mabadiliko katika mfumo wa kimataifa kwa watu wengi zaidi chini ya kauli mbiu “Dunia ya Sawa Inawezekana.”
Hotuba ya Rais Erdogan UN yachapishwa kama kitabu kwa lugha tatu
Hotuba ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan imeangazia zaidi suala la Gaza na kutoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za kimataifa. (AA)

Hotuba ya Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa imechapishwa kuwa kitabu kwa lugha ya Kituruki, Kiingereza na Kiarabu, kuifanya hotuba hiyo kuhusu migogoro duniani na mabadiliko ya kimataifa kuwa machapisho ya kudumu.

Kitabu hicho, kilichozinduliwa na Ofisi ya Rais ya Uturuki siku ya Jumatano, kinaweka pamoja ujumbe wa Erdogan kuhusu Gaza, mizozo ya kikanda, vita vya Urusi na Ukraine na kile alichokieleza kuwa udhaifu katika mfumo wa sasa wa kimataifa. 

Kitabu hicho kimezinduliwa chini ya kauli mbiu ya “Dunia ya Sawa Inawezekana.”

Hotuba hiyo, iliyotolewa jijini New York siku ya Jumanne, iliangazia zaidi Gaza na kutoa wito wa hatua zaidi kimataifa huku akijenga hoja kuwa mfumo wa sasa duniani unahitaji kufanyiwa mabadiliko. 

Erdogan pia alisisitiza kuhusu wito wake wa muda mrefu wa mabadiliko kwa muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, akisema kwa muhtasari kuhusu msimamo wake “Dunia ni Kubwa Kuliko Mataifa Matano”.

Kutoka Gaza hadi utawala bora duniani

Kitabu hicho kinaangazia migogoro ikiwemo Iran, yanayojiri Lebanon na vita vya Urusi na Ukraine, kulingana na ofisi ya Rais.

Zaidi ya mizozo katika nchi, pia inaangazia ugaidi, matatizo ya tabianchi na akili mnemba, kuwasilisha maoni ya Erdogan kuhusu namna mfumo wa kimataifa unaweza kuwa thabiti zaidi katika kukabiliana na changamoto duniani.

Ofisi ya Rais imekieleza kitabu hicho kama muhimu kwa watu kimataifa na vizazi vijavyo, huku muundo wa kuandikwa kwa lugha tatu ukilenga kuufikisha ujumbe wa amani, usalama na maendeleo kwa watu wengi zaidi.

Kitabu hicho kinahitimishwa kwa shairi la Sezai Karakoc

Kitabu hicho kinahitimishwa kwa mizani kutoka kwa mshairi maarufu wa Uturukis Sezai Karakoc, ambaye mashairi yake yanatumika kusisitiza mada za ukweli, historia na uwajibikaji.

Kitabu hicho kinakuja huku viongozi wa dunia wakijumuika jijini New York kwa Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa, huku mapigano Gaza, Ukraine na kote Mashariki ya Kati, pamoja na maswali kuhusu mustakabali wa utawala bora duniani, ukiangaziwa katika agenda ya kimataifa.

Kitabu hicho kinahitimishwa kwa shairi kutoka kwa Karakoc:

“Wanadhani tukinyamaza kimya, suala hilo litasahauliwa.

Ilhali, sisi tukinyamaza, historia haitonyamaza.

Kama historia itanyamaza, ukweli utajitokeza.

Wanadhani wakituondoa, suala hilo litasahauliwa.

Ilhali, wakituondoa, hawawezi kukwepa uwajibikaji.

Hata kama watakwepa uwajibikaji, hawatoepuka adhabu ya historia.

Hata kama wataepuka adhabu ya historia, hawatoepuka adhabu ya Mungu.”

CHANZO:TRT World and Agencies