'Wasiwasi wangu mkubwa sio milipuko:' Baadhi ya wafanyakazi Tehran wanahofia kutolipwa mishahara
ULIMWENGU
5 dk kusoma
'Wasiwasi wangu mkubwa sio milipuko:' Baadhi ya wafanyakazi Tehran wanahofia kutolipwa mishaharaWakazi wengi wa mji wa Tehran tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kabla ya mapigano kuanza.
Wakazi wengi wa mji wa Tehran tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kabla ya mapigano kuanza. / AP
tokea masaa 2

Hivi sasa, kufuatia mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel, mji mkuu wa Iran umekuwa katika hali mbaya zaidi.

Mostafa alikuwa kazini kaskazini mwa Tehran pindi mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel yalipoanza kupiga mji mkuu wa Tehran Jumamosi, siku ya mwanzo ya kazi katika wiki katika nchi yenye idadi kubwa wa Waislamu wa dhehebu la Shia.

Kama ilivyo kwa raia wengi wa Iran, alikuwa tayari kwa mashambulizi ya kijeshi.

Lakini wachache walitarajia mashambulizi ya mchana; walidhani shambulizi lolote lingefanyika usiku.

Baada ya muongo mmoja katika kampuni ya matangazo, Mostafa alijua kuhusu mgogoro huo.

Wakati wa mapigano ya mwaka jana ya siku 12, alifanya kazi akiwa nyumbani ili awe salama.

Mara hii, alikuwa katika meza yake pindi jengo lilipoanza kutikisika.

"Ilishtua," Mostafa ameiambia TRT World, akiomba kutotajwa jina lake la pili kwa sababu za kiusalama.

Mashambulizi yalipopiga mjini, alibaini kuwa hali ya awali ya mgogoro haikufanana na ya sasa.

"Sijuli ilikuwa ni kombora au ndege ya kivita; nilisikia sauti ya filimbi, na madirisha na jengo lote lilitetemeka vibaya. Baada ya sekundi chache, tulisikia milipuko mikubwa karibu."

Wafanyakazi haraka wakaambiwa waende nyumbani.

"Nilikimbia nyumbani.  Nilimtumia ujumbe mke wangu, mama, na baba, kuwajulia hali. Punde, mtandao ukakatwa, na huduma za simu na kutuma ujumbe zikasitishwa."

Mashambulizi ya Marekani na Israel yakiendelea, Mostafa alikuwa katika hali ngumu.

"Wasiwasi wangu mkubwa haukuwa milipuko tu," anasema.

"Mtandao unapofungwa na biashara kufungwa, nilibaini kuwa hakutakuwa na mishahara inapohitajika zaidi."

Kufikia mwishoni mwa Machi 2026, ripoti zinaonesha kuwa zaidi ya watu 3,230 wameuawa Iran, ikiwemo wanajeshi 1,167 na wananchi 1,406, kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Marekani na Israel.

Kupanda kwa bei

Baadhi ya makampuni yaliwasaidia wafanyakazi wake kwa malipo ya mapema, wafanyakazi sita kutoka sekta binafsi wanaiambia TRT World hawajapata chochote kutoka kwa waajiri wao kuhusiana na mshahara wa mwezi Februari na Machi, na wala hawana matarajio ya kulipwa.

Gharama za maisha zinaongezeka Iran.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kituo cha Takwimu za Iran mwezi Februari, hata kabla ya mgogoro wa sasa, mfumko wa bei mwaka kwa mwaka umefikia asilimia 68.1.

Mfumko wa bei kwa mwezi umefikia asilimia 9.4, kiwango kikubwa zaidi katika miaka 3.5.

Inayoshtua zaidi ni mfumko wa bei za vyakula na vinywaji, kwa kupanda hadi asilimia 105.5, kiwango ambacho taasisi za serikali inasema hakijawahi kutokea.

Wakati huo huo, mishahara haipandi.

Razieh, mwenye umri wa miaka 43 mashariki mwa Tehran, amejikuta njia panda katika hali hii ya uchumi.

Bila mkataba wa kudumu, malipo yake ya kila mwezi yanategemea siku anazofanya kazi.

"Hata nilipokuwa nalipwa kwa wakati, ilikuwa ngumu kwangu kuwahudumia watoto watu 3," anasema.

Miaka minne iliyopita, mume wake alipata majeraha makubwa katika moto uliotokea kiwandani na hivi sasa ni mlemavu; familia inapokea fidia ya wastani.

Yeye ndie mlezi wa mtoto wake wa kiume wa miaka 13 na mabinti zake wawili, mwenye umri wa miaka nane na sita.

Shule zimekuwa zikifungwa mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni kutokana na mapigano, na Wizara ya Elimu imetanga kuwa masomo yatafanyika kwa njia ya mtandao mwanzoni mwa Aprili.

Siku za kwanza za mashambulizi, bei ilipanda.

"Katoni ya mayai iliuzwa rasmi karibu na Dola za Marekani 2.  Ilikuwa ni rahisi katika soko la matunda na mboga, lakini siku ya kwanza ya vita, kulikuwa hakuna bidhaa," anakumbuka Razieh.

"Nilienda kununua baadhi 'supermarket,' na walitaka Dola 2.16.  Sikununua. Lakini kitu gani ni rahisi kuliko mayai kulisha watoto?"

Hivi sasa anaishi kwa msaada wa michango kutoka kwa walimu shule na anatafuta kazi ya usafi ili aweze kujikimu.

Ahmadreza, mwenye umri wa miaka 67, anakabiliwa na hali kama hiyo nyuma ya usukani wa gari yake kama dereva wa taksi.

Licha ya hatari zilizopo, bado anaendelea kupenya katika barabara, akitafuta abiria kupitia App maalumu.

"Vita vimefukuza abiria katika mji mkubwa kama huu. Kipato changu kimepungua kufikia nusu ya kile cha mwezi uliopita.  Hivi sasa, maduka yanauza kila kitu ghali zaidi."

Ingawa ana miaka 67, ugumu wa maisha unamfanya aonekane mkubwa zaidi.

Anaendesha akiwa ameinama, akigemea kidogo.

"Kwa vitu kama samaki wa makopo, wenye maduka wanadai aidha wameisha au wanauza kwa bei kubwa maradufu," anasema.

Kodi

Kwa Mostafa, Razieh, na  Ahmadreza, kupata chakula cha kila siku ni sehemu tu ya changamoto; wasiwasi wao mkubwa ni kodi ya nyumba.

Kipato kimepungua au hakipo kabisa kipindi hiki cha vita, lakini majukumu ya kulipa kodi yanabadi pale pale kwa kiwango ambapo sio kwa kawaida tangu kuanza kwa mapigano.

"Tuliposaini mkataba mwanzoni mwa Aprili 2025, nilidhai mimi na mke wangu tungemudu," anasema Mostafa.

"Lakini tulipambana Januari na Februari kwa sababu kukatwa kwa mtandao, na inaonekana tutapata taabu tena mwezi ujao. Na hii ni mwaka huu tu; nani anajua ni kiasi gani kodi itapanda kutokana na mfumko wa bei mwaka huu."

Ahmadreza, anayeishi na mke wake na ana wawili walioolewa, hivi sasa anatumia asilimia 40 ya kipato chake kulipia nyumba ndogo kusini mwa Tehran ambayo haina nafasi ya kutosha kwa ajili ya kukaa na wajukuu zake.

Hofu yake ni kwamba, mgogoro huu usipositishwa, basi anaweza kurudi kijijini katika mkoa wa Saveh, ambapo fursa za maendeleo ni chache.

Mgogoro ni mbaya zaidi kwa biashara ndogo.

Zahra, 29, ametumia miaka 4 kujenga kliniki ya afya ya ngozi.

"Nimepambana kwa miaka minne, naweza kusema nimekuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa. Mwanzoni mwa mwaka huu, nilikuwa nalipa kodi, nalipa mshahara wa wafanyakazi wangu wanne, na napata faida nzuri," ameiambia TRT World.

Hivi sasa, baada ya utulivu kukosekana.

"Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, tumekabiliana na nini? Vita, vikwazo vya kimataifa, na vita tena," anasema.

Kwa sababu biashara yake inategemea zaidi mitandao ya kijamii kuvutia wateja, kukatika kwa mtandao mfululizo kumemfanya ashindwe kufanya kazi.

"Hivi sasa, tunaendesha biashara yetu kwa hasara.  Kodi itaongezeka mwakani, na sitaweza kumudu," anasema Zahra.

Mgogoro unavyozidi, sera za vita vilizotangazwa na serikali ya Iran zinaonekana kulinda maslahi ya umma.

Shirika la Ajira na Utawala la Iran limetangaza kwamba wafanyakazi wa serikali watapokea mishahara yao mapema kuliko kawaida mwezi huu.

Hata hivyo, kwa walio sekta binafsi, serikali imeahidi kuondoa makato ya kodi. Lakini taarifa zaidi ya jinsi utaratibu huo utakavyofanya kazi bado hazijatolewa.

Makala hii imechapishwa kwa ushirikiano na Egab.

CHANZO:TRT World