| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Mkuu wa shirikisho la Afrika aunga mkono Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa AFCON 2027
Rais wa CAF Patrice Motsepe amekiri kuwepo kwa changamoto wakati wa maandalizi lakini akasema CAF imedhamiria kusaidia mataifa hayo matatu kukamilisha yanayohitajika kwa wakati ufaao.
Mkuu wa shirikisho la Afrika aunga mkono Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa AFCON 2027
Rais wa CAF Patrice Motsepe yuko kwenye ziara ya siku mbili nchini Tanzania na Kenya kukagua hatua za maandalizi. Picha / CAF

Patrice Motsepe, rais wa Shirikisho la Soka baranI Afrika (CAF), anasema bado ana matumaini kuwa Kenya, Tanzania na Uganda watafanikisha uwenyeji wa AFCON 2027, akipuuzia uvumi kuwa mashindano hayo yanaweza kupelekwa sehemu nyingine.

Motsepe alikiri kuwepo kwa changamoto wakati wa maandalizi lakini akasema CAF imedhamiria kusaidia mataifa hayo matatu kukamilisha yanayohitajika kwa wakati ufaao.

"Lazima kuwe na changamoto na maeneo ambayo yanahitaji kuimarishwa, lakini tunatakiwa kujiamini kama Afrika Mashariki na Waafrika kuwa tutafanya kazi pamoja na kukamilisha kinachohitajika kwa wakati muafaka," aliwaambia waandishi wa habari siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, Motsepe alikiri kuwa, kazi zaidi inahitajika kufanywa, huku nchi hizo tatu zikijitahidi kukamilisha ukarabati na ujenzi wa miundombinu kabla ya mashindano hayo.

"Nafurahia kazi nzuri inayoendelea nchini Tanzania. Na, imebaki miezi tisa na baadhi ya msisitizo wangu ni kuharakisha kazi hiyo, na tuko hapa kushirikiana, kutoa msaada. Hii ni AFCON yetu."

Michuano ya 2027, ni ya kwanza kuwa na mwenyeji zaidi ya mmoja ambapo Kenya, Tanzania na Uganda, wanatarajiwa kuwa wenyeji kwa mashindano yatakayoanza Juni 19 hadi Julai 17.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Guye na Tigst waongoza Ethiopia kufagia mbio za Berlin Marathon
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani
Mechi za kuwania kufuzu AFCON 2027 zinaanza huku kukiwa na utata kuhusu bingwa mtetezi
Agnes Ng’etich aweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za nusu marathoni za wanawake pekee
Kenya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia 2029 ikiwa ya kwanza barani Afrika
FIFA yakanusha madai ya Morocco ya 'uwenyeji' wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2030
Erdogan akutana na timu ya Voliboli ya wanawake ya Uturuki baada ya ubingwa wa Ulaya
Timu ya wasichana ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 15 imetwaa ubingwa wa CECAFA
Mshambuliaji Aubameyang astaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon
Antonio Rüdiger astaafu kuichezea timu yake ya taifa
Jepchirchir anaongoza ushindi wa 1-2 kwa Kenya jijini Sydney
Gobena avunja rekodi ya Sydney Marathon huku Ethiopia ikitawala mbio za wanaume
Fenerbahce yaifunga Lyon 2-1 kuiwezesha kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya misimu 17
Mkuu wa Shirikisho la UEFA hataki nafasi ya Infantino, anachotaka ni ajiuzulu
Bondia wa zamani bingwa wa dunia Zolani Tete auawa kwa kupigwa risasi nchini Afrika Kusini
Guinea yatangaza nia ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika
FIFA yawaadhibu wachezaji wa Argentina, yaitoza faini shirikisho kwa matukio ya Kombe la Dunia
Cristiano Ronaldo atangaza azma yake ya kustaafu soka
Algeria imefanikiwa kupata medali kwa mara ya kwanza katika mashindano ya WAFCON baada ya kuishinda
Afrika Magharibi ving’ang'anizi kwa mara ya kwanza kwa nafasi ya tatu WAFCON