Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, ameondoka nchini humo Oktoba 6, 2026, kuelekea Uingereza kwa ziara ya kikazi ya siku tano, ambapo atafungua Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania nchini Uingereza.
Wakati wa ziara hiyo, Nchemba anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kukutana wadau, wawekezaji na viongozi wa kampuni mbalimbali katika sekta za madini, benki, Teknolojia, usafirishaji na miundombinu, kwa lengo la kuimarisha na kutangaza fursa za Biashara na Uwekezaji.
Jukwaa hilo litatoa fursa kwa Tanzania kutangaza vipaunbele vya Dira 2050 katika nyanja za uwekezaji na kueleza hatua zinazochukuliwa na serikali kuboresha mazingira ya biashara. Ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwakaribisha, wadau, wawekezaji na wafanya biashara kushiriki katika miradi mbalimbali nchini Tanzania.
Jukwaa hilo limelenga kuvutia mitaji na teknolojia, kukuza ujuzi na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania, pamoja na kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya miundombinu ikiwa ni utekelezaji wa Dira 2050.




















