| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mshambuliaji wa Côte d'Ivoire Wahi hatimaye apata viza ya Canada baada ya kunyimwa awali
Uamuzi huu unakuja baada ya taarifa ya shirikisho la soka kusema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hatokuwepo Canada kwa mechi ya taifa lao dhidi ya Ujerumani.
Mshambuliaji wa Côte d'Ivoire Wahi hatimaye apata viza ya Canada baada ya kunyimwa awali
Wahi alicheza dakika 56 mechi ya kwanza ya Cote d’Ivoire waliopata ushindi 1-0 dhidi ya Ecuador. / Reuters

Mshambuliaji wa Côte d'Ivoire Elye Wahi hatimaye ameruhusiwa kuingia Canada siku ya Alhamisi baada ya kunyimwa viza hapo awali.

Wakitangaza kuwa “tatizo la kiusimamizi” la Wahi limetatuliwa, Shirikisho la Soka la Côte d'Ivoire limesema kwenye mtandao wa X kuwa “Kwa hivyo, mchezaji huyo ameruhusiwa kusafiri na ujumbe wa timu hiyo kwenda Canada na atajumuika kama kawaida pamoja na wachezaji wenzake.”

Uamuzi huo unakuja saa chache baada ya shirikisho la soka kutoa taarifa kuwa mchezaji huyo wa Ligi Kuu ya Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 hatoweza kwenda Canada kwa mechi yao dhidi ya Ujerumani kwa sababu “za msingi za kiusimamizi kwa viza yake ya kuingia Canada kupatikana wakati huu.”

Mwanasheria wa Wahi, Marie Dose, awali alikuwa amesema mchezaji huyo alihojiwa ‘‘kwa saa kadhaa” mwezi uliopita kabla kuachiwa huru.

“Elye Wahi kwa sasa anakabiliwa na mashtaka lakini hajawekewa vikwazo vyovyote na mahakama,” aliongeza.

CHANZO:TRT Afrika Swahili