| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Uwanja wa ndege wa DRC katika eneo lilokumbwa na mlipuko wa Ebola wafunguliwa tena
Uwanja wa ndege wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulioko katika mji mkuu wa mkoa uliokumbwa na mlipuko wa Ebola, umefunguliwa tena, serikali imesema katika taarifa siku ya Jumanne
Uwanja wa ndege wa DRC katika eneo lilokumbwa na mlipuko wa Ebola wafunguliwa tena
Serikali ya DRC imefungua tena uwanja muhimu wa ndege wa Bunia, mji mkuu wa mkoa wa Ituri, kusaidia juhudi za kukabiliana na Ebola. / Reuters

Uwanja wa ndege wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ulioko katika mji mkuu wa mkoa uliokumbwa na mlipuko wa Ebola, umefunguliwa tena, serikali imesema katika taarifa siku ya Jumanne, kubadilisha hatua ambayo baadhi ya raia wanasema iliwawia wao vigumu kupata bidhaa muhimu kutoka maeneo mengine.

Serikali ya DRC ilitangaza mwezi uliopita kuwa inasitisha ndege za abiria katika eneo la Bunia, uwanja mkuu wa ndege mkoa wa Ituri, ambapo maambukizi ya kwanza ya Ebola yalithibitishwa. Ndege za misaada ziliendelea kutoa huduma.

Katika taarifa iliotolewa Jumatatu, wizara ya uchukuzi ya DRC ilisema mazingira sasa yako sawa "kuruhusu huduma kurudi kwa usalama na huduma za usafiri wa ndege" na uwanja wa ndege utafunguliwa tena mara moja.

Wizara inasema abiria wote watapimwa joto kabla ya kupanda kwenye ndege na pia wale wanaowasili, kwamba abiria wanatakiwa kunawa mikono kabla ya kupanda ndege na yeyote ambaye ana homa hatoruhusiwa ndani ya ndege.

Mlipuko huenda ulitokea mapema

Ebola imefika katika maeneo 15 kati ya 36 ya kiafya mkoa wa Ituri, na maambukizi pia yameripotiwa mikoa ya Kaskazini na Kusini na nchi jirani ya Uganda.

Shirika la misaada la Kimataifa la IRC limeonya Jumatatu kuwa mlipuko ulikuwa mkubwa zaidi kuliko vile takwimu rasmi zinavyoonesha.

Shirika hilo la misaada linasema virusi huenda vimesambaa kwa hadi miezi mitatu kabla ya maambukizi ya kwanza kutambuliwa rasmi katikati ya mwezi Mei.

CHANZO:TRT Afrika Swahili