| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania: William Lukuvi kuzikwa Machi 31
Lukuvi alifariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Tanzania: William Lukuvi kuzikwa Machi 31
William Lukuvi enzi za uhai wake./Picha:Wengine
tokea masaa 3

Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi (70), unatarajiwa kuzikwa Jumanne, Machi 31, 2026 katika kijiji chake cha Idodi, Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa.

Lukuvi alifariki dunia Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa leo Machi 26, kesho Ijumaa mwili wake utaagwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, kabla ya Jumamosi kuagwa tena katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Jumapili, Machi 29, mwili huo utasafirishwa kwa ndege hadi Iringa, ambapo Machi 30 utaagwa katika eneo la Gangilonga, kabla ya kupelekwa kijijini Idodi kwa mazishi yatakayofanyika siku inayofuata.

Mazishi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Marehemu Lukuvi, aliyewahi kuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 30 tangu mwaka 1995, ameacha mjane mmoja na watoto watatu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili