Ubelgiji ilifuzu kwa hatua ya timu 16 ya Kombe la Dunia baada ya ushindi 3-2 dhidi ya Senegal siku ya Jumatano, wakifunga magoli mawili dakika za mwisho mwisho kulazimisha muda wa zaida ambapo penati ya Youri Tielemans dakika 125 ilimaliza kazi.
Tielemans alifunga goli hilo la ushindi kwa mkwaju wa penati baada ya kuchezewa rafu ndani ya kumi na nane.
Habib Diarra aliwapa Senegal goli la kwanza katika dakika ya 24. Ismaila Sarr akafanya matokeo kuwa 2-0 katika dakika ya 51.
Ubelgiji kuikabili Marekani
Romelu Lukaku alifunga bao la kwanza la Ubelgiji katika dakika ya 86 kabla nahodha Tielemans kusawazisha mzani dakika tatu baadaye kulazimisha mechi kuingia muda wa ziada.
Ubelgiji itaikabili Marekani Jumanne Julai 7 baada ya timu hiyo kuifunga Bosnia na Herzegovina, huko Seattle 2-0.















