| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Rwanda yafunga zaidi ya viwanda 130 vya pombe haramu
Kwa mujibu wa Utafiti wa Saba wa Demografia na Afya wa Rwanda, asilimia 15 ya wanaume na asilimia 7 ya wanawake hunywa pombe kila siku.
Rwanda yafunga zaidi ya viwanda 130 vya pombe haramu
Watu zaidi ya 50 wanadaiwa kupoteza maisha, na wengine wengi kulazwa hospitalini, baada ya kunywa pombe hizo haramu.

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Rwanda (RFDA) imefunga zaidi ya viwanda 130 vya kutengeneza pombe na kufuta leseni zao kufuatia mzozo mkubwa wa afya ya jamii uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 50 na wengine zaidi ya 100 kupoteza uwezo wa kuona kutokana na pombe haramu na zenye sumu kama methanol.

Watu zaidi ya 50 wanadaiwa kupoteza maisha, na wengine wengi kulazwa hospitalini, baada ya kunywa pombe hizo haramu.

“Tunalichukulia hili kama janga la mlipuko,” alisema Waziri wa Afya wa Rwanda, Sabin Nsanzimana, wakati akizungumza na vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Mwaka 2024, mamlaka nchini Kenya, zilianzisha operesheni ya kitaifa iliyosababisha kufungwa kwa baa na viwanda haramu vya pombe, kuimarishwa kwa masharti ya utoaji wa leseni, na kuanzishwa kwa adhabu kali kwa maeneo yaliyokiuka muda rasmi wa biashara.

CHANZO:TRT Afrika Swahili