| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Tanzania yatangaza kugundua tena gesi asilia Mtwara
Ugunduzi huo ni wa kwanza wa gesi asilia nchini Tanzania katika kipindi cha zaidi ya miaka 10.
Tanzania yatangaza kugundua tena gesi asilia Mtwara
Kwa mujibu wa Waziri wa Nishati, Juma Homera, gesi hiyo imegunduliwa katika kisima cha Kasa-1X ST2. / FB: Juma Zuberi Homera

Tanzania imegundua kiasi kinachokadiriwa kuwa futi za ujazo bilioni 223 za gesi asilia katika eneo la Mnazi Bay, kusini mwa nchi. Ugunduzi huo umetangazwa Jumanne na Waziri wa Nishati, Juma Homera.

Kwa mujibu wa Homera, gesi hiyo imegunduliwa katika kisima cha Kasa-1X ST2, kilichochimbwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni ya nishati ya Ufaransa ya Maurel & Prom.

Ugunduzi huo ni wa kwanza wa gesi asilia nchini Tanzania katika kipindi cha zaidi ya miaka 10.

Homera amesema TPDC na Maurel & Prom zimechimba jumla ya visima vitatu, ambavyo ni MB-5, MS-2 na Kasa-1X ST2. Visima hivyo vinatarajiwa kusaidia kuongeza upatikanaji wa gesi asilia nchini.

Kwa upande wake, Maurel & Prom imesema uzalishaji wa kwanza wa gesi unaweza kuanza mapema mwezi ujao.

Waziri Homera ameongeza kuwa TPDC tayari iko kwenye mazungumzo na wawekezaji wanne wanaopanga kuanzisha miradi ya uzalishaji wa gesi asilia iliyoyeyushwa (LNG) kwa kiwango kidogo.

Kabla ya ugunduzi huu mpya, akiba ya gesi asilia iliyokuwa imegunduliwa nchini Tanzania ilikadiriwa kufikia takribani futi za ujazo trilioni 57.5 katika hali sanifu, kwa mujibu wa mamlaka ya udhibiti wa sekta ya nishati.

CHANZO:Reuters