Watu wapatao 16 wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa baada ya basi kupinduka katika eneo la Western Cape Province.
Kulingana na Idara ya Usimamizi wa Usalama Barabarani ya Afrika Kusini (RTMC), ilitokea usiku wa kuamkia Julai 2, 2026, wakati basi hilo lililokuwa na abiria 78, kupinduka.
Kwa mujibu wa RTMC, basi hilo lilikuwa linasafirisha abiria kati ya mji wa Cape Town kuelekea eneo la Idutywa.
ZILIZOPENDEKEZWA
Jumla ya abiria 20, walipata majeraha mbalimbali ya mwili na kukimbizwa katika hospitali iliyopo mji wa Worcester, huku wengine 43 wakigomea kupata matatibu.
Kulingana na RTMC, uchunguzi wa ajali hiyo bado unaendelea.
CHANZO:AFP











