| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
EU yapiga marufuku ndege kutoka nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania
Kwa mujibu wa taarifa kuhusu orodha ya usalama wa anga ya Umoja wa Ulaya, jumla ya mashirika 87 ya ndege yamehusishwa na vikwazo hivyo.
EU yapiga marufuku ndege kutoka nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania
Marufuko hiyo inatokana na tathmini ya usalama wa anga, na uwezo wa mamlaka za usafiri kufuata viwango vya kimataifa vya usalama. /Air Tanzania

Umoja wa Ulaya (EU) umeweka vikwazo kwa mashirika ya ndege kutoka nchi 12 za Afrika, hatua inayozuia mashirika hayo kufanya safari za ndege kwenda katika nchi wanachama wa Umoja huo kutokana na changamoto zinazohusiana na viwango vya usalama wa anga.

Nchi zilizoathiriwa ni Angola, Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Djibouti, Equatorial Guinea , Eritrea, Liberia, Libya, São Tomé na Príncipe, Sierra Leone, Sudan na Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu orodha ya usalama wa anga ya Umoja wa Ulaya, jumla ya mashirika 87 ya ndege yamehusishwa na vikwazo hivyo.

Hatua hiyo inatokana na tathmini ya usalama wa anga, ikiwemo uwezo wa mamlaka za usafiri wa anga katika nchi husika kusimamia na kuhakikisha mashirika ya ndege yanafuata viwango vya kimataifa vya usalama.

Hata hivyo, baadhi ya mashirika yanaweza kupewa msamaha maalumu baada ya kutathminiwa na mamlaka husika za Umoja wa Ulaya.

Kwa mfano, mashirika mawili ya ndege kutoka Angola, TAAG Angola Airlines na Heli Malongo, yametajwa kutohusishwa na marufuku hiyo.

Kwa Tanzania, hatua hiyo imeibua umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa usalama wa anga ili kuhakikisha mashirika yake ya ndege yanakidhi viwango vinavyotakiwa kimataifa na kuendelea kutoa huduma katika masoko ya kimataifa.