| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
DRC yaaga Kombe la Dunia baada ya kufungwa na England
Mwisho wa safari! Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeaga Kombe la Dunia baada ya kupoteza 2-1 dhidi ya England.
DRC yaaga Kombe la Dunia baada ya kufungwa na England
DRC imeshiriki kwenye michuano ya Komble la Dunia mara mbili, mara ya kwanza ikiwa mwaka 1974. / / Reuters

Mshambuliaji wa England, Harry Kane, alifunga mabao mawili katika dakika za mwisho na kuiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), na hivyo kuitoa kwenye Kombe la Dunia 2026 katika hatua ya mtoano ya timu 32 bora.

Mechi hio iliochezwa Jumatano jijini Atlanta, Marekani, ilianza kwa kasi huku DRC ikitangulia kufunga kupitia bao la Brian Cipenga aliyetikisa nyavu katika dakika ya saba.

Kwa ushindi huo, England imefuzu hatua ya 16 bora, ambapo itakutana na Mexico katika mechi itakayochezwa Jumapili jijini Mexico City.

CHANZO:TRT Afrika