Klabu ya soka ya Uturuki Trabzonspor imetangaza kuwa imeanza mazungumzo na uhamisho na mchezaji nyota wa Misri Mohamed Salah.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye Soko la Hisa la Istanbul na Trabzonspor, klabu hiyo ya Bahari Nyeusi ilisema: "Majadiliano yameanza kwa lengo la kuanza uhamisho wa mchezaji Mohamed Salah, ambaye kwa sasa hana timu yoyote, kwenye klabu yetu."
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alitangaza mwezi Machi kuwa anaondoka klabu ya Ligi Kuu ya England Liverpool FC kufikia mwisho wa msimu 2025-2026.
Salah aliifungia Liverpool magoli 257 katika mechi 442 alizocheza kwenye mashindano yote, na kumfanya kuwa mfungaji wa tatu bora kwenye historia ya klabu hiyo.
Pia amefunga magoli 193 katika Ligi Kuu ya England, 191 akiwa na timu ya Liverpool, kumfanya awe mfungaji wa nne bora akishindwa tu na Alan Shearer, Harry Kane na Wayne Rooney.



















