Rais Recep Tayyip Erdogan ameonya hofu yake juu ya ongezeko la mgogoro wa Iran, akionya kuwa unahatari ya kusambaa katika kanda nzima ya Mashariki ya Kati.
“Mgogoro huu umefikia kiwango cha kutisha, hasa kutokana na mashambulizi ya anga dhidi ya jirani zetu wa Iran,”alisema Erdogan siku ya Alhamisi jijini Ankara.
Kulingana na Rais Erdogan, mashambulizi mengine ya ndege nyuki yanayofanywa na Iran dhidi ya nchi nyingine, yanaibua hofu ya kusambaa kwa mgogoro huo.
Uturuki yaimarisha usalama ikisukuma diplomasia
Kulingana na Rais Erdogan, Uturuki inachukua hatua ya kulinda mipaka na anga yake, ikiendeleza juhudi za kidiplomasia.
“Uturuki haitodharau wala kusita ulinzi wa mipaka na anga zake,” alisema.
“Tutaendelea kusukuma ajenda ya diplomasia kwa nia ya kuzuia umwagaji damu zaidi,” aliongeza Erdogan.
Kiongozi huyo, pia aligusia namna kombora lililorushwa na Iran, lilivyotunguliwa na NATO, akisema kuwa nchi yake ilitoa tahadhari za muhimu kwa nia ya kuepusha tukio kama hilo kujitokeza tena.
“Tutachukua hatua stahiki iwapo usalama wa nchi yetu utakuwa hatarini, kwa kushirikiana na washirika wetu,” alisema.
Migogoro ya kanda yazidi kushamiri
Mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati unaendelea kushika kasi tangu Marekani na Israel ziishambulie Iran, Februari 28.
Shambulio hilo linaripotiwa kuua zaidi ya watu 900, akiwemo aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ali Khamenei.















