| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Somalia lachukua udhibiti wa ngome ya Al Shabab kusini mwa nchi
Jeshi la Somalia limechukua udhibiti wa eneo moja kusini mwa nchi linalotumika kama maficho ya kundi la kigaidi la Al Shabab, Wizara ya Ulinzi ilisema siku ya Jumatano.
Jeshi la Somalia lachukua udhibiti wa ngome ya Al Shabab kusini mwa nchi
Katika miaka ya hivi karibuni, jeshi la Somalia limezidisha kasi katika vita dhidi ya kundi la kigaidi la Al Shabab. / AA
tokea masaa 4

Jeshi la Somalia limechukua udhibiti wa eneo moja kusini mwa nchi ambalo linatumika kama maficho ya kundi la kigaidi la Al Shabab wakati wa operesheni inayoendelea, Wizara ya Ulinzi ilisema siku ya Jumatano.

Wizara inasema vikosi vya Somalia vinajitahidi kuhakikisha eneo la Hawaadley Shabelle ya kati ikiwa ni sehemu ya operesheni Badr iliyoanzishwa na jeshi, ikilenga maeneo yanayotumiwa na magaidi kama “sehemu salama.”

Inasema operesheni hiyo inaendelea kuwasaka magaidi na kuhakikisha eneo hilo liko salama kabisa ambalo hivi majuzi lilikuwa limechukuliwa na kundi hilo lenye uhusiano na Al Qaeda.

Inasema kuwa operesheni hiyo imeharibu ngome kadhaa za Al Shabab na mabohari yao.

Opereshenai dhidi ya Al Shabab inashika kasi

Wizara na uongozi wa jeshi inasisitiza kuwa operesheni dhidi ya ugaidi “itaendelea kushika kasi.”

Wizara ilitangaza Operesheni Rolling Thunder Machi 1, ambayo ni sehemu ya Operesheni pana ya Badr na kuungwa mkono na washirika wa kimataifa, ikiwemo vikosi vya Uganda vilivyo chini ya mwavuli wa AUSSOM.

Al Shabab imekuwa ikijihusisha na ugaidi dhidi ya serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 16, mara nyingi wakilenga maafisa wa usalama, wa serikali na raia.

Tangu mwezi Julai mwaka jana, jeshi la Somalia, kwa msaada wa AUSSOM na washirika wa kimataifa, limeimarisha operesheni dhidi ya kundi la kigaidi.

Muda wa AUSSOM uliongezwa kwa mwaka mwingine mmoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba, huku maamuzi hayo yaliyoungwa mkono na Uingereza yakiongeza muda hadi Disemba 31.

CHANZO:AA