| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Dangote wa Nigeria anasema atalipa kipaumbele soko la mafuta la nyumbani
Kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta cha Dangote nchini Nigeria siku ya Jumatatu kimeahidi kulipa kipaumbela soko la nyumbani kusaidia katika kupunguza uhaba wa mafuta na athari kwa bei za mafuta kutokana na mapigano Mashariki ya Kati.
Dangote wa Nigeria anasema atalipa kipaumbele soko la mafuta la nyumbani
Bei za mafuta nchini Nigeria zimeongezeka kwa asilimia 20% katika kipindi cha wiki moja. / Reuters
tokea masaa 3

Kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta cha Dangote nchini Nigeria siku ya Jumatatu kimeahidi kulipa kipaumbele soko la nyumbani ili kukabiliana na uhaba wa mafuta na kupunguza athari za bei kutokana na mapigano Mashariki ya Kati.

Hata hivyo, imeonya, kuwa hilo linategema kuungwa mkono na serikali na Dangote akasema huenda bei zikapanda tena.

Bei za mafuta katika taifa hilo la Afrika Magharibi tayari zimepanda kwa asilimia 20% katika kipindi cha wiki moja, kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran hukU Iran ikilipa kisasi.

Usambazaji umetatizwa kutokana na mapigano Mashariki ya Kati kufanya bei ya pipa moja kuwa zaidi ya dola $100 duniani Jumatatu, kusababisha hofu ya kuwepo kwa uhaba wa mafuta.

Soko la Kimataifa

Shirika la Mafuta la Nigeria (NNPC) linamilikiwa lote na serikali.

Kuongezeka kwa bei ya mafuta ghafi duniani, gharama za uchukuzi na bima kumesababisha matumizi ya Dangote kupanda.

Bei ya mafuta nchini Nigeria wiki hii imepanda kutoka naira 830 kwa lita moja jijini Lagos hadi naira 1,050 (dola $0.59 to $0.75), ikiwa ni bei ya juu zaidi.

CHANZO:TRT Afrika Swahili