| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Dar kuwaleta pamoja wanahisa wa Afrika
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 1,000 wakiwemo wakuu wa nchi, mawaziri, wawekezaji, taasisi za fedha za maendeleo, viongozi wa sekta binafsi na wataalamu wa miundombinu kutoka Afrika na kwingineko.
Dar kuwaleta pamoja wanahisa wa Afrika
Waziri wa fedha wa Tanzania, Khamis Musa Omar.

Jiji la Dar es Salaam litakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Infra for Africa Forum 2026 na Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Africa50, utakaofanyika Agosti 5 hadi 6 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 1,000 wakiwemo wakuu wa nchi, mawaziri, wawekezaji, taasisi za fedha za maendeleo, viongozi wa sekta binafsi na wataalamu wa miundombinu kutoka Afrika na kwingineko.

Kulingana na waziri wa fedha wa Tanzania, Khamis Mussa Omar, maandalizi ya mkutano huo yanaendelea vizuri, huku ukitarajiwa kuvutia washiriki kutoka ndani na nje ya Afrika, wakiwemo viongozi wa Serikali, taasisi za fedha za kimataifa, wawekezaji, sekta binafsi na wadau wa maendeleo.

Alieleza kuwa mkutano huo unafanyika katika kipindi muhimu ambapo Africa50 inatimiza miaka kumi tangu kuanza rasmi shughuli zake mwaka 2016, taasisi iliyoanzishwa kwa ushirikiano kati ya Serikali za Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya miundombinu barani Afrika.

“Tangu Tanzania ilipojiunga rasmi na Africa50 tarehe 14 Februari 2023 kama mwanahisa wa kundi la nchi za Afrika (African Sovereign States) imenufaika zaidi, hatua iliyopanua fursa za nchi kushiriki kikamilifu katika maandalizi, uendelezaji na ufadhili wa miradi mikubwa ya miundombinu” alisema waziri huyo.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
WHO yatoa wito wa mifumo imara ya afya ili kuimarisha unyonyeshaji watoto
Wafungwa 50 watoroka kutoka gereza la Luebo DRC
Mapigano yakomeshwa kati ya jeshi la Ethiopia na vikosi vya Tigray
Idadi ya waliofariki Ceuta yapanda hadi 72 huku zaidi ya wahamiaji 48,000 wakirejea Morocco
Rais Samia Suluhu Hassan aihimiza Afrika kuondoa utegemezi wa huduma za afya kwa nchi za nje
Tanzania yanyakua ubalozi wa Afrika katika shindano la urembo la 'Miss Supranational 2026'
Iman Elman: Afisa wa Somalia anayeijenga upya nchi kutoka mstari wa mbele
Marekani kufanya sharti la amana ya viza ya dola 20,000 kwa wageni kutoka Afrika kuwa la kudumu
Mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola nchini DRC ni wa pili kwa ukubwa duniani kuwahi kurekodiwa
Sera mpya ya Marekani: Raia wa Malawi lazima wasafiri hadi Kenya kupata viza
Wanamgambo wa RSF wanaojisalimisha wakabidhi vifaa vya kijeshi kwa jeshi la Sudan
Rais wa Liberia Boakai awafuta kazi maafisa baada ya kupatikana kwa dawa za kulevya
Serikali ya Ghana yaunga mkono mapendekezo ya kuongeza muda wa urais
Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua Hospitali ya Mwalimu Nyerere nchini Angola
Nigeria yaharibu silaha haramu 2,819 katika kukabiliana na utovu wa usalama
Besigye: Kutoka daktari binafsi wa Museveni hadi adui wa kisiasa
Uwanja wa Ndege wa Bishoftu nchini Ethiopia: Kwa nini Marekani inakodolea macho mradi huo?
Kenya: Sumu chanzo cha vifo vya tembo wa Amboseli
Mwanasiasa wa upinzani Uganda Besigye alazwa ICU baada ya kuanguka mahakamani: mke wake
Marekani yasitisha huduma za viza katika miji 25 ya Afrika kuanzia Agosti 1, 2026