Mchezaji Djigui Diarra wa klabu ya Young Africans ya Tanzania amefungiwa mitatu na kutozwa faini ya Shilingi 2,000,000 (Milioni 2) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi wa kati katika mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Young Africans, ulioisha kwa sare ya 1-1.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 41:5(5.3) ya Ligi Kuu, kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.
Pia, mchezaji huyo wa kimataifa wa Mali, ametozwa faini nyingine ya Shilingi 2,000,000 (Milioni 2), kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati akitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Wakati huo huo, refa wa mchezo huo, Gilbert Mrina kutoka Kilimanjato, ameshushwa daraja kwa kosa la kushindwa kumchukulia hatua Djigui Diarra kwa utovu wa nidhamu alioonyesha katika mchezo huo.
Refa msaidizi Abdulaziz Ally wa Arusha, amefungiwa mizunguko mitano wa kosa la kushindwa sheria ya kuotea.










