| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Kocha wa Marekani Pochettino akubali kuongeza mkataba kwa miaka 4 hadi Kombe la Dunia 2030
Pochettino ameweka rekodi akiwa na timu ya taifa ya Marekani kwa kushinda mechi nyingi zaidi na kufunga magoli mengi katika Kombe la Dunia 2026
Kocha wa Marekani Pochettino akubali kuongeza mkataba kwa miaka 4 hadi Kombe la Dunia 2030
Kocha wa timu ya taifa ya Marekani Mauricio Pochettino.

Shirikisho la Soka la Marekani limetangaza siku ya Jumatatu kuwa Mauricio Pochettino amekubali kuongeza mkataba wake kama Kocha wa timu hiyo ya taifa hadi wakati wa Kombe la Dunia 2030.

Shirikisho lilieleza hilo kuwa “ukurasa mpya katika mradi ambao utampa nafasi kocha Pochettino na benchi lake la ufundi kuendelea kuimarisha Timu ya Taifa ya Wanaume ya Marekani wakati wakiwa na uwezo wa kulipa nguvu soka la Marekani kwa ujumla” katika taarifa kwenye mtandao.

“Mauricio na benchi lake la ufundi wanaamini kuhusu mustakabali wa soka la Marekani na mradi wetu mpya unatoa nafasi wa kuimarisha USMNT na kutilia nguvu soka la Marekani,” alisema Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirikisho ambaye pia ni Katibu Mkuu JT Batson.

Akieleza kuhusu uwezo wa timu ya Marekani, Pochettino alisema “Hamasa tulioona kutoka kwa mashabiki wakati wa Kombe la Dunia imetia nguvu imani yetu kwa kile ambacho kinachowezekana. Tunafurahia fursa hii ya kufikisha ujuzi na utaalamu wetu katika maeneo mbalimbali Marekani wakati huohuo tukiimarisha uwezo wa wachezaji, makocha na timu zilizoko chini ya shirikisho.”

Baada ya kuanza kuinoa timu hiyo 2024, kocha huyo raia wa Argentina ameweka rekodi ya timu ya taifa ya Marekani kwa kushinda mechi nyingi zaidi na kufunga magoli mengi katika Kombe la Dunia 2026.

CHANZO:َAA