Ajali ya helikopta Magharibi mwa Kenya siku ya Jumamosi ilisababisha vifo vya watu sita, ikiwa ni pamoja na mbunge, taarifa za polisi na maafisa wa serikali zilisema.
Helikopta hiyo ilianguka katika Kaunti ya Nandi, eneo la North Rift.
Sababu haikujulikana mara moja. Kamanda wa polisi wa kaunti hiyo Samuel Mukusi aliambia kituo cha televisheni cha Kenya Citizen TV kwamba mbunge huyo, rubani na watu wengine wanne wamefariki.
Rais William Ruto alimtaja mbunge huyo kuwa ni Johana Ng'eno, wa eneo bunge la Emurua Dikirr, katika chapisho kwenye ukurasa wake wa X. Ng'eno, 53, alihudumu kama mbunge tangu 2013, baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka huo, na tena 2017 na 2022.
Ruto awapa pole familia ya marehemu, marafiki
“Mawazo na sala zetu ziko pamoja na familia yake, marafiki zake, watu wa Emurua Dikirr, na waathiriwa na familia zote zilizoathiriwa na ajali ya helikopta huko Mosop, Kaunti ya Nandi,” Ruto aliandika.
Abiria wengine hawakutambuliwa mara moja.









