Na Paschalin Mbenge Basil
Matumaini ya bara la Afrika yako wazi. Na fursa ya kutekeleza hilo pia inaonekana.
Kutoka kwa Mpango wa Biashara Huru Barani (AfCFTA) hadi Agenda 2063, bara hili lina mipango kabambe ya ukuaji, ushirikiano wa kikanda mabadiliko ya kiuchumi. Serikali zinaimarisha mabadiliko ya sera, wawekezaji wanajitokeza na taasisi zinaunga mkono juhudi za bara kuwa pamoja.
Wakati Afrika ikiendelea kuwa kitu kimoja, moja ya mawazo yake ya muda mrefu huenda yakawa msingi muhimu zaidi: Ubuntu. Msingi wake, Ubuntu unatambua kuwa maendeleo yanajengwa kwa watu kushirikiana, kuaminiana na maelewano kuwa mafanikio yetu yanakuwepo kutokana na mafanikio ya wengine.
Katika bara la Afrika ambalo mataifa yanaunganika zaidi, Ubuntu siyo tu suala la kitamaduni. Ni mfumo ambao unaweza kuleta maendeleo.
Utekelezaji wa wa Ubuntu
Ushirikiano wa hivi karibuni kati ya shirika la Kenya la Pesalink na mfumo wa malipo barani wa PAPSS unaonesha mfano wa namna mustakabali utakavyokuwa. Kwa kuwezesha mfumo wa malipo wa haraka, wa bei nafuu kati na kwa kutumia sarafu za nchi za Afrika, kunaondoa vikwazo kwa biashara katika kanda na kusaidia kutimizwa kwa mpango wa AfCFTA.
Lakini teknolojia pekee haiwezi kufanya mfumo kama PAPSS kufanikiwa. Inategemea serikali, waratibu, taasisi za fedha na wawekezaji kushirikiana, kuaminiana na kuwa na dhamira ya lengo la pamoja.
Kwa njia nyingi, huo ni utamaduni wa Ubuntu.
Waziri wa taifa fulani anapofanya majadiliano kuhusu makubaliano ya biashara anafaa kuwa na mawazo zaidi ya nje ya nchi yake. Mkurugenzi wa kampuni anayesimamia mfumo wa usambazaji kati ya nchi kadhaa. Maafisa wa umma wanatarajiwa kuhudumu katika idara mbalimbali za serikali, huku mashirika ya kiraia yakiendelea kushirikiana na serikali pamoja na wafanyabiashara katika kutatua changamoto za pamoja.
Uongozi siyo kusimamia shirika moja. Ni kuhusu, kuendeleza Ubuntu katika taasisi mbalimbali, sekta na mipaka na kutatua matatizo ambayo hayawezi kutatuliwa na sekta au nchi moja pekee.
Kugundua kuwa uwezo utategemea siyo tu sera mahsusi na uwekezaji, lakini viongozi ambao watawaleta watu pamoja, kuimarisha taasisi na kufanya matarajio kuwa na matokeo thabiti.
Na ndiyo maana ya kuwa na mradi wa Uongozi wenye Tija barani Afrika (TAL), ulioanzishwa kwa ushirikiano wa Idara ya Utawala Bora ya Nelson Mandela katika Chuo Kikuu cha Cape Town, Chuo Kikuu cha Mohammed VI nchini Morocco, Chuo Kikuu cha Cheikh Anta Diop Senegal na Taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
TAL imeanzishwa kwa msingi wa: Mustakabali wa Afrika unahitaji uongozi unaoratibiwa na uhalisia wa bara la Afrika.
Mpango huu wa TAL unadhihirisha matarajio kuwa bara la Afrika linaweza kuzalisha viongozi inayotaka kwa kuangazia elimu yake wenyewe, utamaduni na uzoefu wake. Kama Ubuntu inavyotukumbusha, maendeleo ya kudumu yanajengwa kwa watu kushirikiana. Kwa kuwekeza kwa viongozi hao sasa, Afrika inawekeza kwa mustakabali wake.
Mwandishi , Paschalin Mbenge Basil, ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika miradi ya utekelezaji mbalimbali kwenye masuala ya maendeleo nchini Kenya, Afrika na duniani. Bi Basil anasimamia miradi ya utafiti na ushirikiano wa kimkakati ndani ya taasisi ya Mafunzo ya Maendeleo katika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

















