Philippe Lazzarini , Kamishna mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA anasema hali Palestina inazidi kuzorota/  Picha by UNRWA

Philippe Lazzarini , Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA anasema kuwa vifo vinazidi kuongezeaka Gaza.

"Tunapozungumza, watu huko Gaza wanakufa. Wanakufa tu kwa mabomu na mashambulizi . Hivi karibuni, wengi zaidi watakufa kutokana na matokeo ya kuzingirwa kwa Ukanda wa Gaza," Lazzarini amesema katika mkutano wa waandishi wa habari Mashariki mwa Jerusalem.

Takwimu za hivi punde zinaonyesha kuwa waliokufa hadi sasa ni 8,836: ikiwa Wizara ya Afya ya Israela inasema Waisraeli 1400 wamekufa na Wizara ya Afya ya Palestina ikisema watu 7,326 wamekufa Gaza na 110 katika eneo la West Bank.

Matamshi ya Lazzarini yanaonekana kukanusha yale ya rais wa Marekani Joe Biden ambaye ndani ya juma alisema haamini idadi ya Wapalestina waliokufa iliyotolewa na Wizara ya Afya ya Palestine iko sawa.

Alisema kuwa, "hana dhana kwamba Wapalestina wanasema ukweli kuhusu idadi ya watu waliouawa."

Lazzarini anasema watoa huduma pia wanalengwa katika mashambulizi ya Isarel dhidi ya Gaza.

"Leo, angalau wenzangu 53 wamethibitishwa kuuawa. Kwa siku moja, tulipata uthibitisho kwamba 15 waliuawa," Lazzarini ameongezea.

" Kila siku inazidi kuwa siku ya huzuni kwa Umoja wa Mataifa na UNRWA huku idadi ya wenzetu wanaouawa ikiongezeka."

Kamishna huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya Palestine, anasema 'hakuna anayeweza kudai "sikujua", huku picha, na sauti za mateso yasiyoelezeka zikiendelea kutoka kila saa kutoka Gaza.'

" Hatuwezi tena kufumbia macho mkasa huu wa kibinadamu. Mamilioni ya watu wanauliza, hasa katika eneo hili, hata zaidi katika Gaza, "Kwa nini ulimwengu hauna nia ya kuchukua hatua na kukomesha jehanamu hii duniani?" Wanastahili jibu."

TRT Afrika