Majukumu ya kijasusi kwa wanyama na ndege yanaonekana kupata thamani kubwa kutokana na kuibuka kwa teknolojia mpya. / Picha: AP

Nyangumi aina ya beluga ambaye alishukiwa kufanya ujasusi nchini Urusi baada ya kuonekana katika maji ya Norway miaka mitano iliyopita amepatikana akiwa amekufa, kwa mujibu wa shirika lisilo la faida ambalo lilikuwa likimfuatilia nyangumi huyo.

Mwili wa Hvaldimir - jina la kimzaha la Wanorway kwa kuashiria uhusiano wa nyangumi huyo na rais Vladmir Putin - ulipatikana ukielea kusini mwa Norway mwishoni mwa juma, shirika la utangazaji la Norway NRK liliripoti.

Hvaldimir alikuwa amevalia mshipi wenye kile kinachoonekana kuwa ni kilindi cha kamera ndogo alipopatikana kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 karibu na kisiwa cha Ingoya kaskazini mwa Norway.

Nyangumi huyo alipendezwa sana na watu na aliitikia ishara za mikono, jambo lililosababisha shirika la upelelezi la ndani la Norway kudhani kwamba alikuwa amezuiliwa nchini Urusi kama sehemu ya mpango wa utafiti kabla ya kuvuka bahari ya Norway.

Sio mara ya kwanza

Hii, hata hivyo, haikuwa mara ya kwanza kwa wanyama kutumiwa kwa upelelezi, mojawapo ya taaluma kongwe zaidi duniani.

Wakati utumiaji wa wanyama na ndege katika vita vya kale, kuanzia mbwa wa kunusa hadi njiwa za wajumbe, umerekodiwa kvyema katika kumbukumbu, majukumu ya kisasa ya upelelezi yanaonekana kuwa na thamani kubwa na mchanganyiko wa teknolojia.

Njiwa -kama-jasusi ilianza 1907, wakati Julius Neubronner alipounda kamera ndogo ya kiotomatiki ili kuwafunga ndege wake. Ugunduzi wake uliafungua njia kwa njiwa zilizo na kamera kutumiwa na jeshi la Ujerumani wakati wote wa Vita vya Kwanza vya Dunia.

Wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu na Vita Baridi vilivyofuata, wapelelezi wenye mabawa, hasa mwewe, kunguru na njiwa, walipewa mafunzo na mashirika ya kijasusi kwa ajili ya ujasusi.

Mnamo 1976, Marekani iliweka wazi hati ya Ofisi ya Utafiti na Maendeleo ambayo ilitoa mwanga juu ya jaribio la kutoa mafunzo kwa aina mbalimbali za ndege katika kazi ya kukusanya taarifa za kijasusi kwa ajili ya misioni ya usaidizi, hasa Ulaya.

Ripoti hiyo pia ilisifu njiwa kwa kuwashinda wanyama wengine wote katika ujasusi. Njiwa wamepata medali nyingi za heshima kuliko mnyama mwingine yeyote katika historia ya kijeshi na akili.

Katika miaka ya 1960, CIA ilijaribu hata kutumia dolphins wenye shingo ndefu kwa mashambulizi ya chini ya maji dhidi ya meli za adui na kwa ufuatiliaji.

Kulingana na ripoti za hivi karibuni, jeshi la Israeli linaunda na kutoa mafunzo kwa "roboti za nyoka" kushughulikia maeneo magumu na yaliyozuiliwa kwa misheni za kijasusi.

Mnamo mwaka wa 2016, tai mkubwa mwenye mabawa ya futi sita alivuka mpaka wa Israeli na kuingia Lebanon. Wenyeji walishuku mnyama huyo alikuwa akitumiwa kuwapeleleza kwani alikuwa na kifaa cha kielektroniki kilichowekwa kwake.

Ushindani wa kijasusi kutumia njiwa umekuwa wa kawaida katika bara dogo la India, ambapo wapinzani wakuu India na Pakistan 'wamemkamata' Njiwa kwa kosa la ujasusi, mara nyingi vikiibua mfululizo wa meme za kufurahisha kwenye mitandao ya kijamii.

Mnamo Mei 2015, India ilimkamata njiwa mweupe katika eneo linalozozaniwa la Kashmir ambaye inadaiwa alitoka Pakistani na mnamo Oktoba 2016, njiwa mwingine aliwekwa chini ya ulinzi baada ya kupatikana na barua ya kumtishia Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.

Mnamo Mei 2020, mwanamume kutoka Pakistani aliandika barua ya hisia kwa Waziri Mkuu wa India akimtaka amrudishe Njiwa wake. Polisi wa India, hata hivyo, walisema njiwa huyo alikuwa na pete kwenye mguu wake mmoja, iliyoandikwa code ambazo walikuwa wakijaribu kung'amua.

Mwanamume huyo kutoka Pakistani alidai kuwa njiwa aliyekamatwa hakuwa na msimbo bali nambari yake ya simu ya mkononi.

Hivi majuzi, mnamo Februari 2024, mamlaka ya India ilimwachilia njiwa porini baada ya kumweka katika 'kizuizini' kwa miezi minane kwa sababu alishukiwa kufanya ujasusi kwa Wachina.

TRT World