'Tuliambiwa wazi kwamba hata ikiwa mshukiwa anaingia kwenye jengo lenye watu ndani yake, tunapaswa kufyatua risasi kwenye jengo hilo na kumuua gaidi, hata ikiwa watu wengine watajeruhiwa' asema mwanajeshi wa Israel ? Picha :Reuters 

Maafisa na wanajeshi wa Israel wamekiri kwamba wengi wa waliouawa waliotajwa na jeshi kama "magaidi" wakati wa vita vyake dhidi ya Gaza ni raia, ripoti imesema.

Gazeti la Israel la Haaretz lilikusanya ushuhuda kutoka kwa maafisa na wanajeshi ambao wamepigana huko Gaza wakati wa vita, ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu Oktoba 7, 2023.

"Jeshi la Israel linasema magaidi 9,000 wameuawa tangu vita vya Gaza kuanza," ripoti hiyo ilisema.

Maafisa na wanajeshi wa Israel, hata hivyo, waliiambia Haaretz kwamba "mara nyingi hawa ni raia ambao uhalifu wao pekee ulikuwa kuvuka mstari usioonekana unaochorwa na jeshi la Israel."

"Tuliambiwa wazi kwamba hata ikiwa mshukiwa anaingia kwenye jengo lenye watu ndani yake, tunapaswa kufyatua risasi kwenye jengo hilo na kumuua gaidi, hata ikiwa watu wengine watajeruhiwa," askari mmoja aliambia gazeti hilo.

TRT World