Uturuki inakaribisha kuanzishwa tena kwa shughuli za Ubalozi wa Azerbaijan katika mji mkuu wa Iran Tehran.
"Tunazingatia kuhalalisha uhusiano kati ya Azerbaijan na Iran, na kurejeshwa kwa uhusiano wa kidiplomasia katika kiwango cha kawaida kama muhimu kwa utulivu wa eneo na moyo wa ushirikiano," Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema mapema Jumanne.
Ubalozi wa Azerbaijan mjini Tehran ulianza tena kazi yake siku ya Jumatatu baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mazungumzo kati ya nchi hizo mbili ili kupunguza mvutano, ripoti za vyombo vya habari zimesema.
Afisa katika ubalozi huo amesema kuwa umeanza tena shughuli zake lakini tangazo rasmi la Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran bado linasubiriwa.
Shambulio la ubalozi
Uhusiano kati ya Iran na Azerbaijan umeshuhudia panda na shuka kwa miaka mingi.
Mvutano uliongezeka baada ya shambulio la Januari 2023 kwenye ubalozi katika mji mkuu wa Iran, ambapo mtu mwenye silaha alivamia ujumbe huo na kumuua afisa wa usalama anayesimamia na kujeruhi wengine wawili. Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev alikashifu kitendo hicho kuwa ni "kitendo cha kigaidi."
Azerbaijan iliwaondoa wafanyikazi wake na wanafamilia kutoka kwa misheni baada ya shambulio hilo na pia imewashauri raia wake dhidi ya kusafiri kwenda Iran.