Shirika la Afya Duniani linasema hali Gaza inazidi kuzorota

Shirika la Afya Duniani linasema hali Gaza inazidi kuzorota

WHO inalaani vikali shambulio la hospitali ya Al Ahli Arab kaskazini mwa Gaza.
WHO imelaani shambulio katika hospitali Gaza / Picha: Reuters

Shirika la Afya Duniani , WHO inasema kuwa hali ya kibinadamu katika eneo la Gaza inazidi kuzorota.

"Kila sekunde tunaposubiri kupata msaada wa matibabu, tunapoteza maisha," mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom amesema.

"Kwa siku nne vifaa vya WHO vimekwama mpakani. Tunahitaji ufikiaji wa haraka ili kuanza kutoa vifaa vya kuokoa maisha. Tunahitaji vurugu kila upande kukomeshwa," Adhamon ameongezea.

WHO inalaani vikali shambulio la hospitali ya Al Ahli Arab kaskazini mwa Gaza.

Taarifa ya Tedros Inasema hospitali hiyo ilikuwa ikifanya kazi, ilikuwa na wagonjwa, watoa huduma za afya na wahudumu, na wakimbizi wa ndani.

Ripoti za mapema zinaonyesha zaidi ya watu 500 wameuawa pamoja na majeruhi.

Hospitali hiyo ilikuwa mojawapo ya hospitali 20 kaskazini mwa Gaza zinazokabiliwa na maagizo ya kuhamishwa kutoka kwa jeshi la Israel.

Agizo la uokoaji halijawezekana kutekelezwa kwa kuzingatia hali ya sasa ya ukosefu wa usalama, hali mbaya ya wagonjwa wengi, na ukosefu wa ambulensi na wafanyakazi.

TRT Afrika