Fidan anasema mpango wa Trump wa kuhama Gaza 'haukubaliki,' hata kuufungua kwa majadiliano ni makosa. / Picha: AA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amelaani vikali pendekezo la hivi mkaribuni la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwaondoa Wapalestina kutoka Gaza na kusema kuwa "halikubaliki".

"Hata kufungua mjadala kama huo ni makosa," Fidan alisema Jumatano, akithibitisha kupinga kwa Uturuki kwa mpango wowote unaotaka kuwaondoa watu wa Gaza kutoka kwa nchi yao.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumanne kwamba Marekani "itachukua udhibiti" wa Gaza, muda mfupi baada ya kupendekeza makazi mapya ya kudumu ya Wapalestina nje ya eneo hilo.

"Marekani itachukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza, na tutaifanyia kazi," alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu.

Kuhusu Syria, Fidan alisisitiza kuwa Damascus haina mipango ya kutoa mamlaka kwa maeneo mingine, akisisitiza tena kwamba serikali ya Syria itadumisha uadilifu wa eneo lake.

"Msimamo wa Rais wa Syria al Sharaa kuhusu kundi la kigaidi la PKK/YPG uko wazi kabisa na unaendana na malengo ya usalama ya Uturuki," aliongeza.

Fidan aliendelea kubainisha kuwa Syria imeahidi kuwafukuza au kuwakata makali magaidi wote wa PKK ambao wameingia nchini humo kutoka mataifa mbalimbali ili kuhifadhi umoja wake wa kitaifa.

Pia ametangaza mipango ya utaratibu wa pamoja kati ya Uturuki, Iraq, Syria na Jordan ili kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh.

TRT World