#KXQ84 : تسعة قتلى جراء تدافع في ملعب بالسلفادور (الشرطة) / Photo: AFP

Watu 12 wameuawa katika mkanyagano kwenye uwanja wa El Salvador ambapo mashabiki wa soka walikuwa wamekusanyika kutazama mashindano ya ndani, polisi walisema.

Mamlaka zilisema ripoti za awali ziliashiria msongamano wa mashabiki waliojaribu kuingia katika Uwanja wa Cuscatlan katika mji mkuu wa San Salvador wa Amerika ya Kati kutazama mechi kati ya timu za Alianza na FAS.

"tuna taarifa mabaya za awali za waliopoteza maisha 12, tisa ambao wako hapa uwanjani na wengine watatu ambao tumearifiwa wako katika vituo tofauti vya hospitali," mkurugenzi wa Polisi wa Kitaifa (PNC) Mauricio Arriaza aliwaambia waandishi wa habari.

"Soka ya Salvador iko katika maombolezo," Arriaza alisema.

Mechi hiyo ilisitishwa huku wahudumu wa dharura wakiwaondoa watu kutoka uwanjani  Picha AP

Carlos Fuentes, msemaji wa kundi la huduma za dharura Comandos de Salvamento, alisema walikuwa wakiwahudumia zaidi ya watu 500.

"Takriban watu 100 waliokuwa katika hali mbaya walipelekwa hospitalini, huku wengine wakionyesha dalili za kukosa hewa na aina nyingine za kiwewe", Fuentes alisema.

Mkanyagano huo unaonekana ulianza baada ya lango la uwanja kuanguka na kusababisha watu kujaa pamoja, aliongeza.

Mechi hiyo ilisitishwa huku wahudumu wa dharura wakiwaondoa watu kutoka uwanjani hapo, ambapo mamia ya maafisa wa polisi na wanajeshi walikusanyika huku ving'ora vya gari la wagonjwa vikilia.

Reuters