Israeli imedhibiti kivuko cha Rafah upande wa Gaza mwezi Mei wakati wa mashambulizi yake ya ardhini katika mji wa Rafah na kukasirisha Misri ambayo ilisema itaacha kushirikiana na Israeli kwenye suala muhimu la uingizaji usaidizi ndani ya eneo hilo. /Picha: AP

Maafisa kutoka Marekani, Israeli na Misri wamemaliza mkutano mjini Cairo, huku Misri ikishikilia msimamo wake kwamba Israeli lazima iondoke upande wa Palestina wa kivuko cha Rafah ili iweze kufanya kazi tena, duru za usalama zilisema.

Vyanzo viwili vya usalama vya Misri vilisema, mkutano wa Jumapili ulikuwa mzuri licha ya kuwa hakuna makubaliano ya kufungua tena kivuko hicho.

Ujumbe wa Misri katika mkutano huo ulisema inakaribisha wazo la kuingia kwa waangalizi wa Ulaya kwenye mpaka huo kusimamia operesheni ya mamlaka ya Palestina ikiwa mamlaka ya Palestina itakubali kurejea kazini.

Maafisa wa Israel na Marekani walisema watafanya kazi haraka ili kuondoa vikwazo katika uendeshaji wa kivuko hicho, duru za Misri zilisema.

Israeli ilidhibiti kivuko upande wa Gaza mwezi Mei, wakati wa mashambulizi yake ya ardhini katika mji wa Rafah, na kukasirisha Misri ambayo ilisema itaacha kushirikiana na Israel kwenye suala muhimu la kuingiza usaidizi ndani ya eneo hilo na kuwahamisha watu kutoka humo.

Inagawaje Misri iliwezesha kuingia kwa msaada kupitia kivuko cha Karem Abu Salem wiki iliyopita, kufunguliwa tena kwa Rafah ni muhimu kwani mashirika ya kibinadamu yanaonya juu ya njaa inayokuja huko Gaza.

TRT World