Balozi Jeff Flake alitoa maoni hayo wakati eneo hilo likijiandaa na mashambulizi yanayoweza kufanywa na Iran / Picha: AP

Marekani inamwomba Uturuki na washirika wengine ambao wana uhusiano na Iran kuishawishi kupunguza mvutano katika Mashariki ya Kati, balozi wa Marekani nchini Uturuki alisema.

Balozi Jeff Flake alitoa maoni hayo wakati eneo hilo likijiandaa kwa mashambulizi yanayoweza kufanywa na Iran na washirika wake baada ya mauaji ya wanachama waandamizi wa kundi la Hamas na Hezbollah.

Iran imeungana na Hamas kuilaumu Israeli kwa mauaji ya Ismail Haniyeh, kiongozi wa kisiasa wa kundi la Palestina. Israel haijatoa kauli ya kuhusika.

"Tunawaomba washirika wetu wote ambao wana uhusiano wowote na Iran waweze kuishawishi na kupunguza mvutano, washirika hao ni pamoja na Uturuki," Flake alisema katika meza ya duru na waandishi wa habari huko Istanbul anapokaribia kuhudumu kwake kama balozi wa Marekani nchini Uturuki.

"Wanafanya wawezavyo ili kuhakikisha kwamba hauzidi kuongezeka," alisema kuhusu wapatanishi wa Uturuki na Washington, akiongeza kwamba "wanaonekana kuamini zaidi kuliko sisi kwamba hautazidi kuongezeka".

Flake alibainisha "nafasi muhimu" ambayo Uturuki ilikuwa imetekeleza katika mabadilishano makubwa ya wafungwa kati ya Marekani na Urusi tangu Vita Baridi yakyofanyika mjini Ankara mwanzoni mwa Agosti.

Katika mahojiano na Reuters mwezi Juni, Flake alisema kuwa Uturuki imesalia imara katika nchi za Magharibi na ushirikiano wake na Marekani umezidi kuwa na nguvu.

TRT World