Mahakama ya kupambana na ugaidi , ATC, mjini Islamabad imetoa dhamana kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan katika kesi nyingi.
Khan, ambaye ana zaidi ya kesi 100 zilizowasilishwa dhidi yake tangu kuondolewa mamlakani mwaka jana mwezi Aprili, alisafiri hadi mji mkuu Islamabad kufika mbele ya ATC siku ya Jumanne.
ATC ilitoa dhamana kwa Khan katika angalau kesi nane hadi Juni 8, kulingana na watangazaji wa Pakistani.
Akiwa amesidikizwa na mkewe Bushra Bibi, Khan sasa anatazamiwa kufika mbele ya shirika la kupambana na ufisadi Ofisi ya Taifa ya Uwajibikaji, NAB, katika kesi inayohusu kesi ya Al Qadir Trust.
Kulingana na Farrukh Habib, msaidizi wa Khan na kiongozi wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf, PTI, kuna "takriban kesi 150" zilizowasilishwa dhidi ya Khan.
Nchi hiyo ya Asia Kusini imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kisiasa tangu kuondolewa madarakani kwa Khan kupitia kura ya kutokuwa na imani naye Aprili 2021.
Khan amedai uchaguzi wa haraka, ambao vinginevyo umepangwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Anakabiliwa na wingi wa kesi ambazo wafuasi wake wanadai kuwa zimechochewa kisiasa.
Alikamatwa na NAB, idara ya kupambana na ufisadi nchini humo, kuhusiana na madai ya ufisadi yanayohusisha Taasisi ya Chuo Kikuu cha Al Qadir. Hata hivyo, kukamatwa kwake kulitangazwa kuwa kinyume cha sheria na mahakama kuu ya nchi hiyo na baadaye kuachiliwa kwa dhamana.
Inadaiwa Khan na mkewe Bushra Bibi walipokea mabilioni ya pesa na kipande kikubwa cha ardhi ya gharama ya kujenga taasisi hiyo ya elimu kwa malipo ya kutoa kiasi cha paundi milioni 190 (dola milioni 236) kwa tajiri wa mali mnamo 2020.
Kiasi hicho kilitambuliwa na kurejeshwa nchini na Shirika la Kitaifa la Uhalifu la Uingereza kufuatia suluhu na tajiri Malik Riaz mnamo 2019.
Idara ya kupambana na ufisadi inadai kuwa serikali ya Khan ya PTI ilifanya makubaliano na Riaz ambayo yalisababisha hasara ya zaidi ya dola milioni 239 kwa hazina ya kitaifa katika mpango wa quid pro quo na mfanyabiashara huyo.
Khan na viongozi wa chama chake, hata hivyo, wamekanusha madai hayo.
Pia aliponea chupuchupu kuuawa wakati wa maandamano ya mwezi Novemba mwaka jana.